November 2, 2018

Ulimwengu Wa Wamasoni (2)

Imetafsiriwa na Naaswir Haamid


Bwana Rudyard Kippling ni Mmasoni mwengine ambaye ni mwandishi marufu wa riwaya ya "The Jungle Book", ameandika kitabu kinachoitwa "The Man Who Would One Day be King". Kitabu hichi badaye kikaingizwa katika bajeti kubwa ya Hollywood, wachezaji wakuu wakiwa ni Sean Connery, Michael Kane na Saeed Jaffery. Kitabu hicho ni hadithi ya askari wawili wanaofunga safari ya kwenda sehemu za mwisho za India. Nchi ambayo hapo kale ilikuwa ikisemwa mno kwa kuwa na matajiri wakubwa ambao walitokana na Mkuu Alexander. Walipofika nchi hiyo, askari wawili hawa wanakamatwa na wenyeji wanaotambulika kwa jina la Kafir walioitwa kutokana na nchi yao ya Kafiristan. Pale wanapokaribia watu wawili hao kuuawa, kidani kinaonekana shingoni mwa askari mmoja kikiwa na alama ya Jicho Moja La KimasoniKafir hao wanampa heshima ya mungu wao na kumsifia kwamba ni mwenye kuishi milele. Mtu mwenyewe hapo mwanzo alijisifia kwamba ni Mfalme na badaye anatambua nguvu mpya ndani yake binafsi inayomtambulisha kwamba ni mungu.

Kwa mujibu wa elimu ya Uislamu kama sio imani nyenginezo pia, mfano unaooneshwa kutokana na hadithi hiyo unastajabisha kweli kweli. Maandiko ya Kiislamu yanayoitwa Hadiyth yana simulizi nyingi za Utume wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ndani ya Hadiyth hizi, zinaeleza kwamba kutatokea mtu miongoni mwa Kaffir ambalo ndani ya Uislamu lina maana ya wasiomuamini Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), mtu huyu atatambulikana kwa Jicho lake Moja na atafanywa kuwa ni Kiongozi wa Dunia, mwanzo akidai kuwa ni Mfalme na baadaye kuwa ni mungu atakayeaminika kuishi milele hadi wakati wake aliowekewa (na Mola).

Katika mchezo mwengine, dhana ya kiongozi wa dunia na serikali moja pia inatiliwa mkazo mno katika hila za propaganda. Mnamo mwaka 1996, mchezo wa "Indepencence Day" ulivunja rikodi ya mauzo kwa kushikilia nafasi ya juu ya saba miongoni mwa michezo yote ya wakati wote. Mchezo huo unaoneshwa kwa dunia nzima ambao una hadithi ya kutunga kuhusu uvamizi wa kiumbe cha majabu ulimwenguni Alien. Hata hivyo, ndani kabisa ya mchezo huo kuna ujumbe uliojificha unaoweza kupatikana, unaoonesha kuwepo kwa Umasoni na agenda za Kimasoni. Ndani ya mchezo huo, kuna ngome ya kijeshi inayoitwa "Area 51" ni hapa ambapo mashambulizi yanaanza kufanywa na ni ngome hii ambayo dunia nzima na viumbe vyengine vyote inaitegemea. Mlango wake wa kuingilia umetengenezwa kwa aina ya pyramid (pembe tatu) na ambao umechongwa kwa alama ya Jicho Moja.
Mchezo huo unaonesha kwamba USA ndie mpiganaji mkuu dhidi ya uharamia huo unaohusisha mataifa mengine duniani. Uharamia ambao umevumbuliwa, kuongozwa na kuamrishwa na mtu mmoja – Kiongozi mkuu mmoja. Mchezo huo ni sehemu kuu ya upanuzi wa michezo na vipindi vya runinga katika mada za viumbe vya ajabu, UFO na uvamizi unaohatarisha maisha ya mwanaadamu ulimwenguni. Michezo kama hii inaitia hamasa jamii kufuatilia mada hizi. Hizi ni miongoni mwa njia nyingi zinazotumiwa na Wamasoni katika kutengeneza njia ya serikali moja. Wamasoni wanatumia aina nyingi za kuingiza khofu ndani ya mioyo ya watu, ikiwatia hamasa ya kuwa na haja ya ulinzi wa hali ya juu na hivyo kuwa na haja ya usalama wa ziada. Haja ya usalama na ulinzi zinaweza tu kutimizwa kwa kuwa na serikali moja ya Ulimwengu mzima ikilinda matakwa ya wanaadamu wote duniani. "Kwa hakika iwapo tutakutana na tishio la uvamizi wa kiumbe cha maajabu kutoka nje ya dunia, nafikiria kwamba ndivyo itatumiwa sababu hiyo kuzifuta kabisa tofauti zetu duniani kwa haraka, na bora nikuulize kwani bado hakuna nguvu za kiumbe wa maajabu miongoni mwetu?"

Njia nyengine wanazotumia Wamasoni ili kufanikisha serikali moja ya dunia nzima na haja ya kuwepo ulinzi wa dunia unaoongozwa na wao ni kuruhusu kuongezeka kwa makosa ya jinai hadi kufikia kiwango cha kutisha. Kwa kutumia njia hii, wanasababisha kuwepo kwa khofu ya kuhitaji usalama binafsi na wa taifa.

Uzalishaji wa madawa ya kulevya kwa mujibu wa maofisa unakadiriwa kwa mujibu wa makadirio ya fedha kuwa ni uzalishaji mkubwa kabisa duniani. Nchi tofauti hivi sasa zinajitahidi kusuluhisha tatizo hili katika ngazi za kitaifa na kimataifa. Kwa mfano USA ina tatizo baya kabisa na linaloongezeka pale unapozungumzia kuhusu madawa ya kulevya. Kinachoonekana ndani ya USA ni kwamba makosa ya jinai yanaongezeka katika kiwango cha juu kabisa. USA inasukumwa na malalamiko na madai ya wananchi kuitaka serikali kuchukuwa hatua kali, iwapo kwa kipigo cha dhahiri au siri kupambana na tatizo la madawa ya kulevya na kuridhisha maoni ya jamii. Hata hivyo, takwimu zinazoumiza kichwa kuhusiana na uzuiaji wa madawa ya kulevya nchini Marekani zinatia shaka kuhusiana na uwezo na msukumo wa serikali hiyo. Inaaminika kwamba mnamo miaka ya 1960, aliyekuwa mwenyekiti wa FBI Bwana J. Edgar Hoover, aliruhusu biashara ya madawa hayo kutumika ndani ya jamii ya Wamarekani Weusi (African American) katika jaribio lake la kudumaza harakati za watu weusi nchini Marekani.

Mnamo miaka ya 1980 pamoja na tishio la ukomunisti kuchukua hatamu Marekani ya Kati, pesa zilihitajiwa haraka kugharamia harakati za wanamgambo dhidi ya ukuaji wa ukomunisti. Na ili kufanikisha hili, CIA iliruhusu madawa ya kulevya kufanyiwa biashara ndani ya Marekani.  Hili linadhihirishwa kutoka kwa American Senator Bwana Jack Bloom ambaye alikuwa ni mjumbe wa kamati ya uchunguzi katika suala hilo.

Tokea hapo kale, Wamasoni wamekuwa wakitumia au wakibuni matatizo ndani ya jamii ili kugeuza na kuharibu matokeo kwa mujibu wa agenda zao. Ongezeko la tatizo la madawa ya kulevya nchini Marekani linawaridhia viongozi kutumia nguvu za aina zozote kwa wakati wanaotaka. Usafirishaji baina ya Atlantic American na Latin American tayari umeshawekwa chini ya uangalizi.

Haitochukuwa muda mrefu kabla ya kuwepo haja ya kutumia nguvu za pamoja ulimwenguni. Miongoni mwa mambo yanayoridhia lengo la kuwepo uendeshaji wa watu ni uharibifu wa habari za kweli na matumizi ya kutumia uzalishaji na takwimu za upande mmoja ambazo ni zana za serikali za Kimasoni za leo, kubuni haja ya uma katika ulinzi wa hali ya juu kitaifa na kimataifa, kuongeza idadi ya makosa ya jinai, madawa ya kulevya na kuongeza matendo ya ugaidi. Maendeleo katika teknolojia ndio inayowapatia uwepesi Wamasoni kufanya walitakalo, teknolojia hii inaruhusu matendo ya watu wote kuwepo chini ya uangalizi, kuchunguzwa na kuhifadhiwa.

Ufunguo wao ni kuwa na kila aina ya taarifa. Kila taarifa zinapoongezeka kuhusu watu ndipo wanapoweza kutabiri uhakika wa matendo yao na namna wanavyofikiri na inakuwa kwao rahisi kuwaongoza katika uharibifu na bila ya kujielewa. Wamasoni wanaziendesha jamii na mahitaji wanayoyahitaji, lakini kwa kutumia ulaghai wa teknolojia daima zipo kukuzuia yale unayoyataka na yale unayoyachagua, hakika ni ukweli wa uzalishaji wao na namna wanavyoharibu akili za watu. Njia ambazo zimetumiwa kuendesha upande unaoamuliwa kuuongoza watu na njia hizi ambazo zinadhibiti kila nyanja ya maisha ya mwanaadamu, na njia hiyo ndio maisha yako!!!

Vitendo vya kutisha kama vile vya ugaidi, ongezeko la makosa ya jinai, ongezeko la hujuma vyote hivi vina mzizi wake kutoka vyombo vya habari. Na kwa upande mwengine serikali nayo inatengeneza mazingira ambayo itaridhiwa kutumia mabavu, kuweka zana za kuchunguza mienendo ya watu. Teknolojia zaidi na zaidi zinavumbuliwa ili kuwachunguza watu, hali hii inaongezeka hadi kufikia kwamba ni serikali ya kibeberu tu ndio inafaidika na uchunguzi huu. Mawazo ya watu kwa mara nyengine yanageuzwa ili kuwapa Wamasoni ridhaa ya matendo yao na kuwarahisishia yale malengo yao. Hivi sasa tayari teknolojia ipo mbioni ya namna za kuchunguza watu na kuhifadhi maelezo binafsi ya watu ndani ya jamii kwenye sehemu ya kuhifadhia takwimu nyingi. Harakati zinavyozidi ndivyo inavyochukua nafasi ya kuhifadhi maelezo binafsi ya watu katika kifaa kidogo cha plastiki kama vile maelezo ya benki, leseni ya udereva na bima ya taifa. Inaonesha kwamba maelezo haya hivi sasa yanafanyiwa kazi ili kuyaunganisha pamoja katika kadi moja tu. Matokeo yake itakuwa ni kuchunguza hali zote za watu katika manunuzi na maelezo binafsi ya watu kwa kutumia kidole (on a click).

Mnamo mwaka 1992 Makamo Mwenyekiti wa Mahkama Kuu ya Uingereza Bwana Nicholas Brown Mulkinson alieleza kwamba iwapo polisi watapewa mamlaka ya kukusanya katika sehemu moja taarifa kuhusu kodi za ardhi, huduma za jamii na afya na huduma nyenginezo, basi uhuru wa mtu utakuwa hatarini. Watakuwa tayari wanaweza kutambua nani unazungumza naye kwenye simu, wapi unafanya kazi, wapi unafanya manunuzi yako, nini unakula, nini unavaa, unatumia gharama za aina gani, maingizo yako na orodha hii inakwenda mbele na mbele zaidi. Kadi moja tu inaweza kuruhusu uchunguzi wa karibu zaidi na kuwezesha kupatikana maelezo ya kina ya akili ya kila mtu katika jamii. Taarifa ambazo zinafanya wepesi kuagua udhibiti wa kuharibu matendo ya watu. Hata hivyo, kuna pengo ambalo Wamasoni wanahitaji kuliziba kwa kuondosha matumizi ya sarafu isiyotumia umeme (hard currency). Sarafu hizi ambazo zinatumiwa zaidi duniani, zinaweza kumfanya mtu kukimbia uchunguzi na kuhifadhiwa maelezo yake kwa njia ya teknolojia. Hili ni kwa sababu manunuzi ya sarafu hizi hayawezi kufuatiliwa kwa kina.

Kutokana na hili, harakati zinafanywa za kuondosha sarafu isiyotumia umeme kwa mtindo ambao zitakuwa zinategemea moja kwa moja katika kutumia umeme. Kwa maneno mengine, mfumo huu unaoetegemea moja kwa moja matumizi ya kadi, uchunguzi na udanganyifu umekamata alama za mwanzo katika harakati za kuanzisha kadi malumu na fedha za umeme nchi nzima ndani ya Uingereza. Mpango wa mondex ni wa mwanzo kutoka benki za magharibi na British telecom na ubunifu wa mwanzo wa kuanzisha kadi malumu. Ndani ya kadi hii kuna micro chip ambayo inaweka kumbukumbu ya kila manunuzi, sio tu ya pesa bali inahifadhi kila aina ya kitu kinachotumiwa. Inaweza kufanya kazi kama ni credit card, paspoti ya jamii, kadi ya maktaba, kadi ya kusafiria, kadi ya simu na bila ya shaka kadi ya utambulisho. Dhana ya kadi hii malumu imebuniwa kutoka Ufaransa ambayo ina mfumo wa kibabe katika kuhifadhi taarifa za watu.

Ingawa kadi ya utambulisho inaweza kufungua mlango wa maelezo mengi, hakika haitakuwa na uwezo wa kumuonesha wapi mtu alipo katika wakati fulani. Hili litahitaji kuwepo mfumo malumu wa kifaa cha kufuatilia mwenendo wa mtu ambacho kinaweza kuwekwa ndani ya kadi hiyo na kumfuatilia popote alipo duniani. Kifaa cha kufuatilia mwenendo wa mtu kinaweza kuwa ni kifaa kiduchu cha utambulisho au kifaa kinachotumia umeme ndani ya kadi. Vifaa kama hivi vinatumika kupasha habari ambazo zinachukuliwa na satellite kwenye low earth orbit ikimuonesha na kumtambua muhusika.

Ingawa kazi hii inaweza kuonekana kama ya uongo, hata hivyo inafanyiwa kazi hivi sasa kuwa ni ya kweli. Hivi sasa kuna takribani satallite 48 ulimwenguni ambazo zinatumika na Marekani na washirika wake. Satellite hizi zinaweza kupewa amri kwa kutumia alama (signals) na kusafirisha taarifa sahihi kutoka chanzo kinachohitajika. Kwa wakati wa sasa, chanzo cha signals hizi ni vifaa vilivyomo katika matanki, ndege na meli za vita au hata zana za mkononi kwa malengo ya kupata picha ya ramani iliyo sahihi kabisa. Hatua inayofuata itakuwa ni kuanzisha kifaa ambacho kitatoasignal asili kutoka kwa kila mtu.


Hivi sasa mfumo mmoja wa kifaa hicho ambacho kimevumbuliwa mahsusi kama nisignal asili kwa ajili ya satellite ni electronic tag. Huu ni mpango ambao unatumika Uingereza. Sababu ya kufanya hili ni kwamba inahitajika kwenda sambamba na ongezeko la idadi ya watu ndani ya jela zilizosheheni watu. Tag hii inavalishwa kwenye mkono wa wanaotiwa hatiani na wanaweza kufuatiliwa kuangalia iwapo watiwa hatiani hao wanakiuka amri za kuzima taa jioni (curfew).

Matumizi ya tag kwa marubani pia inafanyiwa kazi huko Manchester, Bark Shaw na Norfolk kwa mipango ya kutumika tag hii nchi nyenginezo huko mbele. Ndani ya makala katika gazeti la Daily Telegraph la tarehe 13/11/1997, Jack Straw aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza amenukuliwa akisema kwamba electronic tag imetumika sana miaka iliyopita na matokeo yake watu wengi zaidi wanaridhika nacho. Hakuna mjadala kwamba kiini haswa cha mpango huu kwa maendeleo ya watu huko mbele imetumia jicho lao lililo makini na kwamba Wamasoni hivi sasa wanaweza kutia nguvu zaidi mipango yao ya kuiendesha dunia wakiiharibu kwa mujibu wa matakwa yao na uharibifu huu utafanikiwa kwa namna yoyote.

Wamasoni wanapanga mikakati madhubuti kuuendesha ulimwengu kwa kutumia serikali moja, na hivyo ni lazima watengeneze njia ya uchumi wa aina moja, utungaji wa sheria wa aina moja, siasa moja na jeshi la dunia nzima. Mnamo tarehe 25 ya Machi mwaka 1957, iliundwa Jumuiya ya Uchumi barani Ulaya European Economic Community EEC, hatua hiyo ni ya mwanzo katika kuanzisha serikali moja. Tokea hapo kale, EEC imekuwa ni uwanja wa majaribio kwa ajili ya mwenendo mpya duniani – new world order.


Kwa msingi wa kanuni za uhuru wa kutembea baina ya wajumbe wa nchi shirikishi, tayari wameanzisha bidhaa na watu ambao wanaweza kutembea huru kabisa ndani ya taifa hili kubwa. Mipango ipo mbioni kuanzisha mfumo mmoja wa uangalizi na harakati za kuanzisha serikali moja ya Ulaya zinapanda juu kila siku na hivyo kusafisha njia kwa ajili ya siasa moja na utungaji mmoja wa sheria. Yote haya yana maana kwamba hapo badaye ndani ya taifa hili kubwa la EEC kutakuwa na sarafu moja, uchumi mmoja na serikali moja na bila ya shaka serikali wenyewe ni lazima iwe ya Kimasoni.


Wachejaji watatu wakuu wa EEC ni Uingereza, Ufaransa na Ujerumani. Uingereza na Ufaransa tokea hapo zamani zimekuwa ni nchi zinazoongozwa na Umasoni. Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, Ujerumani ilishirikishwa moja kwa moja na Uingereza na Ufaransa pamoja na Marekani ambalo ni taifa jengine la Kimasoni na Umoja wa Kisovieti. Nyanja ambazo zilikuwa zikidhibitiwa na nchi tatu hizo zilizotajwa ni za Kimasoni, zilizotengeneza utambulisho mwengine wa kisiasa unaoitwa Ujerumani ya Magharibi na kutokana na kuporomoka kwake ukuta wa Berlin huko Magharibi ya Ujerumani imechukuliwa na Mashariki ya kale ya Ujerumani.

Ulaya haipo peke yake katika jitihada za kufanikisha hadhi ya mataifa yenye nguvu kubwa. Marekani na Mexico hivi sasa ndizo nchi mbili tu za Makubaliano ya Biashara Huru Marekani ya Kaskazini (NAPHTHA –North American Free Trade Agreement). Hata hivyo, mataifa ya Kusini yanaendelea kushajihishwa kujiunga na umoja huo. Kwa kuwepo mataifa makubwa ya Kimasoni ndani ya Ulaya na Marekani, umoja ulio imara utakuwa ndio dhana sahihi na maendeleo mepesi. Hata hivyo, kuna tatizo jengine ambalo Wamasoni wanahitaji kupambana nalo iwapo wanataka kuwa mabwana wa ulimwengu mmoja.

Ilipofika miaka ya 1970, ilikuwa inadhihirisha wazi kwamba idadi ya Wazungu na Wamarekani weupe inapunguwa kwa kasi. Hili liliwatia khofu na juhudi zilihitajika kulitafutia ufumbuzi, kwani kuachiwa kuendelea kuna maana ya kwamba idadi kubwa ya watu katika mataifa ya ulimwengu wa tatu yatahatarisha usalama wa kitaifa wa nchi zinazodhibitiwa na Wamasoni. Manunuzi ya Magharibi na uzalishaji wake yatapunguwa na matokeo yake mataifa haya yatakuwa yanategemea moja kwa moja kwa watu wa ulimwengu wa tatu. Kwa upande mwengine, pengo baina ya watu wa Magharibi na idadi ya watu wa dunia ya tatu lilihitajika kujazwa ili kurudisha hadhi ya juu ya Magharibi au kwa lugha sahihi hadhi ya Kimasoni ulimwenguni.

Mnamo miaka ya 1970, raisi Jimmy Carter aliunda kamisheni ya dira ya ulimwengu wa 2000, ripoti hiyo ililaumu matatizo yote kuwa yanatokana na ukuaji wa idadi ya watu wasio kuwa weupe. Ripoti hiyo ilikwenda mbali hadi kushauri udhibiti wa idadi ya watu angalau bilioni mbili ndani ya mataifa ya ulimwengu wa tatu hadi kufikia mwaka 2000. Hili lilishauriwa ili kurudisha hadhi ya juu ya Magharibi. Maajabu kwamba pia ndani ya miaka ya 1970, janga la UKIMWI likaripuka na kuchukuwa idadi kubwa kabisa ya maisha ndani ya mataifa ya ulimwengu wa tatu na halikadhalika ndani ya watu weusi na Wahispania kutoka Marekani.


Ilisemwa kwamba kirusi cha UKIMWI kilitokana na kima wa rangi ya kijani ndani ya Afrika na badaye kilisambazwa kwa wenyeji iwapo ni kwa matendo ya kinyama au matumizi ya chakula.

Hata hivyo, simulizi hiyo ilikuwa ni ndogo kinyume na ukweli wenyewe.Mnamo tarehe 2 ya Juni mwaka 1988, gazeti la Los Angeles Times lilichapisha makala iliyokataa maelezo ya kwamba kirusi cha mwanaadamu cha UKIMWI kimetokana na kima wa rangi ya kijani. Makala hiyo ilifichua ushahidi kwamba DNA kutoka kwenye virusi haishabihiani hata kidogo na kima hao. Bila ya shaka itatambulika kwamba virusi vya UKIMWI haviwezi kuonekana sehemu yoyote ya asili na vinaweza tu kuishi ndani ya mfumo wa kutengenezwa wa kuhifadhi baiolojia wa mwanaadamu – human biological system.

Iwapo kirusi hicho hakikuibuka kutokana na viumbe, suala linakuja wapi kiliibuka na ni wapi hakika kirusi hichi kilitoka mzizi wake? Mnamo tarehe 4 ya Julai mwaka 1984, gazeti la New Delhi nchini India linaloitwa Patriot lilichapisha makala inayoonesha kwa mara ya kwanza kwamba madai ya UKIMWI yanapingana na baiolojia. Mtaalamu wa utabibu wa wanyama kutoka Marekani ambaye hakudhihirisha jina lake, ameyanukuu madai ya UKIMWI kuwa yametengenzwa kitaalamu kutoka maabara ya kijeshi ya Marekani huko Ford Detrick karibu na Frederick. Baadaye mnamo tarehe 30 ya Oktoba mwaka 1985, gazeti la Kisovieti la Liternia Gazetta lilirudia madai yaliyochapishwa na gazeti la Kihindi na kusababisha mgogoro wa kimataifa. Hata hivyo, zogo lote hili la chanzo cha kirusi cha UKIMWI liliondoshwa na Wamasoni wa Kimagharibi kama lilivyoondoshwa taifa babe la Kikomunisti.

Mnamo tarehe 26 ya Oktoba mwaka 1986, gazeti la Sunday Express lilikuwa ni gazeti la mwanzo la Kimagharibi kuweka habari kwenye ukurasa wake wa mwanzo kuthibitisha hitimisho walilokuja nalo magazeti ya Kihindi na Kisovieti walilolipa jina la "UKIMWI umetengenezwa ndani ya maabara".Ndani ya makala hii, kwa wakati na nafasi tofauti Dr. John Seal na Prof. Jacob Seagall ambaye ni mkurugenzi mstaafu wa idara ya baiolojia katika Chuo Kikuu cha Berlin, walimaliza na maelezo kwamba kirusi cha UKIMWI ni cha kutengenezwa na mwanaadamu.

Uripukaji wa UKIMWI umeunganishwa na mipango ya kutoa chanjo ulimwenguni.Gazeti linaloheshimika kimataifa la London Times lilichapisha makala ukurasa wa kwanza mnamo tarehe 11 ya Mei mwaka 1987 yenye kichwa cha habari "Chanjo ya Suruwa Yagundulika kuwa na UKIMWI". Makala hiyo inaunganisha baina ya chanjo ya suruwa iliyofanywa na Jumuiya ya Afya Duniani kwa takribani watu milioni 50 – 70 ndani ya nchi tofauti Afrika ya kati na kule kuibuka kwake UKIMWI ndani ya maeneo hayo. Jumuiya ya Afya Duniani ni tawi la kiafya la Umoja wa Mataifa.

Ushahidi huo unaonesha kwamba UKIMWI ni virusi vilivyoenezwa kupitia zoezi la kufanya chanjo ndani ya ulimwengu wa nchi za tatu. Ni kirusi kibaya dhidi ya watu wasio na hatia na wanyonge kwa lengo la kudhibiti idadi ya watu duniani.

UKIMWI si chochote zaidi ya suluhisho la kisasa na yote haya yanafanywa kwa lengo la kupenyeza sera ya kiuchumi ambayo itaruhusu utegemezi wa ulimwengu mzima kwa Wamasoni wa Magharibi. Hata hivyo kuhodhi uchumi kwa Wamasoni peke yake halitoshelezi. Ili kuwezesha serikali ya Kimasoni kutimiza malengo yao ambayo itakuwa ndio jumuiya ya ulimwengu mzima chini ya udhibiti wa Kimasoni na uchumi mmoja wanahitaji kuwa na jeshi moja, na hakuna shaka yoyote kwamba umoja huo ni wa Umoja wa Mataifa - UN.

Ufaransa na Marekani tayari zina nafasi ya juu ndani ya mataifa makuu ya Baraza la Usalama na wengine wakiwa ni Urusi na Uchina. Hili lina maana kwamba wana nguvu tosha kuruhusu tendo lolote linalohitaji kupitishwa - VITO. Mnamo Disemba ya mwaka 1992, raisi wa Baraza Kuu alitangaza kwamba UN ni lazima iwe na bunge lake la dunia nzima na aliendelea kusema kwamba UN ni lazima iwekewe huduma zake malumu za kiusalama.

Hata hivyo, UN hivi sasa imeshakuwa na nguvu za kijeshi. Inafanya kazi kama ni jeshi. Jeshi ambalo lilikaa nyuma wakati maelfu ya Waislamu walipouliwa na Waserbia huko Bosnia na badala yake wakacheza mchezo wa kuzuia silaha ambao uliwaacha Waislamu kutokuwa na himaya yoyote. Majeshi ya UN yaliwahi kupelekwa kupigana vita dhidi ya Kamanda Muhammad Farah Idiid kipindi cha baina ya miezi Juni na Oktoba mwaka 1993. Na matokeo yake ni kwamba helikopta za Kimarekani zilishambulia hospitali, nyumba na makundi ya watu. Yakiuwa mamia ya watu wasio kuwa na silaha waliovamiwa na ambapo watu 71 waliuawa. Juu ya yote mkuu wa kitengo cha malengo ya UN bwana Admiral Jonathan Howard alisema: "Tulitambua nini tunapiga, tulipanga vizuri."

Tendo hili hakika lilikuwa ni kinyume na makubaliano yaliyofanyika Geneva – Geneva Convention. Lakini pale alipoendewa mwanasheria wa jeshi la Marekani kuhusiana na dondoo hizi, jibu lake lilikuwa kwamba makubaliano ya Geneva hayafanyi kazi kwa majeshi ya UN. Utetezi wake kwa njia ya kijanja ni kwamba UN sio mtiaji saini wa makubaliano hayo.

Kwa maneno mengine ni kwamba majeshi ya UN yalikuwa huru kutenda jinai za vita (war crimes) au kuuwa namna wanavyopenda na walikuwa juu ya sheria. Ukweli ni kwamba UN, mbali na kuleta (msaada wa) vyakula kama wanavyodai, wametandaza ubadhirifu ardhini wakiacha athari ya vifo na maangamizi popote inapokwenda. Zimeondoka siku za vita baridi ambapo Umoja wa Kisovieti ulikuwepo kila mahala na ambapo fikra za Kimasoni za serikali moja zilichukuwa muda kufanikiwa. Sasa kwa vile Ukomunisti umemalizwa, inaonesha kuwa Wamasoni angalau wanaweza kuwatumia UN kufanikisha malengo yao ya serikali moja ulimwenguni.

Kutokana na kuihodhi dunia nzima ndani ya mikono yao na akiwa hayupo wa kuzuia wanapotaka kwenda, hivi sasa Dunia inatoa kilio kwa sababu ya ubadhirifu na unyama waliyoyatandaza ardhini kupitia karne zao za kutisha za kuuhodhi ulimwengu. Ingawa wanaona kwamba hakuna wa kupingana nao, lakini Dunia inashuhudia kuja tena majeshi yaliyopo huko kabla. Sasa hivi Wamasoni wana adui mwengine wa kupambana naye, adui ambaye hapo kabla walidhani kwamba wameshammaliza. Adui ambaye daima hatasalimu amri dhidi ya ubadhirifu na mipango ya kinyama ya Kimasoni. Adui huyo ni Uislamu na dhidi yake wametangaza vita.

Inaendelea in Shaa Allaah...

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only