November 2, 2018

Ulimwengu Wa Wamasoni (3)

Imetafsiriwa na Naaswir Haamid


Hata hivyo, tokea hapo zamani, Waislamu wamekwisha tahadharishwa kuhusiana na adui ambaye watakutana naye. Mjumbe wa mwisho wa Allaah Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba kuna mtu atatokea baada ya Waislamu kuuteka mji wa Kirumi unaoitwa Constantinople. Awali atatokea kama ni mfalme mbabe baadaye atadaiwa kuwa ni mtume na mwishowe watu watadai kuwa ni mungu. Tayari hatua ya mwanzo ya utume imeshatimizwa. Constantinople tayari imetekwa na kubadilishwa jina la Istanbul. Mtume amesimulia zaidi kwamba muongo huyu ataanza kuiteka dunia. Nchi baada ya nchi, ngome baada ya ngome, mkoa baada ya mkoa, mji baada ya mji na kutakuwa hakuna sehemu yoyote inayoweza kukimbilika isipokuwa Miji Mikuu Mitakatifu ya Makkah na Madiynah. Atamiliki nguvu za kuiamrisha mbingu kunyesha mvua nayo itatii, na ardhi kuchipua nayo itazalisha mazao. Atawalingania watu kwenye dini ya uongo na kuwaletea kitu kinachofanana na pepo na moto, lakini kile kinachoonekana kama ni pepo hakika ni moto na kile kinachoonekana kama ni moto ukweli ni kwamba ndio pepo. Huyo ni Dajjaal mwenye maana ya kafiri na atazaliwa akiwa na jicho moja na Mola wenu sio jicho-chongo!! Pia inajulikana kwamba, kabla ya kutokea Dajjaal, kikundi cha watu kitatayarisha njia wakitengeneza mbinu tofauti kuitayarisha dunia kwa ajili ya kuwasili kwake. Kwa maneno mengine hawa watangulizi wake Dajjaal na miundo yao watafanana na kila sifa za Dajjaal na yeye atakuwa ndio mwenye kuhitimisha hiyo mitindo na alama zisizokuwa za kibinaadamu. Watangulizi wake wakuu wa Dajjaal sio wengine isipokuwa ndio Wamasoni. Hilo jicho moja ndio njia za kumtambua Dajjaal, nalo jicho moja ndio alama ya Wamasoni. Ni miongoni mwa imani zao na imetolewa kutoka kwenye hekaya za kale za Kimisri. Katika dhana zao, linamaanisha ukubwa, kwa mara nyengine likihusishwa kana kwamba ndilo lenye kuusanifu ulimwengu.

Wanachuoni wa Kiislamu wanasema kwamba mfano unaoshabihiana na Dajjaal ni kama ule wa Firauni aliyepelekewa Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam). Firauni alikuwa ni kiongozi mbabe aliyejipandisha hadhi ya juu na kujitangaza kuwa ni mungu. Alitumia wachawi kufanya hadaa na kuwadanganya watu, aliwanyanyasa watu wote waliokwenda kinyume na dini yake ya kiongo. Hivi leo, Wamasoni wameunga aina nyengine ya uchawi. Hadaa wanazotengeneza, zinachukua mfumo uliojificha au hata ujumbe wa wazi wa kipropaganda ndani ya michezo, runinga, katuni, miziki na kila zana nyenginezo zilizobandikwa vyema katika vyombo vya habari. Na vyombo hivi hivi vimeendelea kutumiwa kutukana na kubomoa Uislamu. Vikiendelea kwa mtindo mwengine wa biashara ya Dajjaal anayekwenda mbali na kumtukana Mungu moja kwa moja. Dajjaal ni mnyanyasaji wa kila asiyemfuata. Atakuwa na nguvu kuongeza au kuharibu ardhi inayohitaji kuvunwa akiegemeza na maoni ya watu wanaotaka kumfuata. Halikadhalika, Wamasoni wa Kimagharibi kupitia Benki ya Dunia – World Bank wanahodhi rehani ya mataifa ya ulimwengu wa tatu iwapo hawatofuata matakwa yao. Dhilali ya IMF iliyojaa mikopo ya maendeleo, kawaida inatumiwa kuhakikisha kuyabana mataifa kama hayo na riba isiyolipika ikiwabana kisawasawa. Wanalazimishwa kujisalimisha au kukutana na kuanguka uchumi wao na kusababisha kufa njaa. Njia nyengine itakayotumiwa na Dajjaal katika kuwaendesha watu aidha kwa kuwalaghai au kuwalazimisha kujisalimisha ni kwa kueneza maradhi. Atakuwa na uwezo wa kueneza au kuponya maradhi. Hakika atakuwa na nguvu kama za mungu na kwa kutumia nguvu hizi atawaburuza wengi katika dini yake ya uongo. Wamasoni nao wanacheza na maisha ya watu katika mtindo kama huo. Ushahidi upo unaonesha kwamba virusi vingi vimetengenezwa au kuvumbuliwa ndani ya maabara ya kijeshi. Baadaye virusi hivi vilitumika kuwafanyia majaribio wanadamu, na inatambulika kwamba UKIMWI ni zana ya mwanadamu inayotumika kutimiza malengo ya Kimasoni wa Magharibi.

Dajjaal atajaribu kumchana chana Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika Sifa Zake zote na kuzitumia yeye. Mabavu haya ndio njia za Wamasoni ambao wanatumika kuibadilisha Sheria ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa ile iliyotengenezwa na mwanaadamu, huku wakidai kueneza uadilifu ndani ya ardhi na wakitumia teknolojia kuangalia yote unayofanya na huku wakijaribu kusikia kila kitu. Wakitumia elimu ya uzazi kubadili na kutengeneza maumbile (ya ajabu) ili kufikia viwango vyao vya uongo. Hawa ndio watangulizi wa Dajjaal na ndio Wamasoni.

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba kutakuja wakati dunia yote itaungana kupanga mikakati ya kuwamaliza Waislamu kama mfano wa wanavyokutana kwenye meza kula chakula. Hivi leo, mataifa ya dunia nzima yanafanya kama hivyo wakizunguka meza ya duara ya Umoja wa Mataifa kupitia ukumbi wa Baraza Kuu. Pia amesema kwamba wakati atakaokuja Dajjaal utakuwa ni wakati wa akili kufadhaika ambapo watu wataamini uongo na kukataa kile kilichokuwa ni kweli na wale wanaofanya mikakati ya kumpinga Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) watakuwa na mdomo katika maisha ya watu. Leo hii wakati unaosuburiwa kuja Dajjaal pia kuna mambo ya fadhaa. Mtindo unaotengenezwa na watangulizi umewatoa Waislamu wengi mbali na ukweli wakitumia utajiri na anasa na kuwatimizia matakwa ya Ulimwengu.  Huo ni usaliti wa aibu kabisa. Wakati huu wa dhiki ni mfano wa jitu kubwa likiwatenga Waumini wa kweli mbali na makafiri na wanafaiki. Wengi wametumia mtindo wa maisha na dhana za mtindo wa Dajjaal wakibakia pengine na hilo jina la Kiislamu au kivazi, wakivaa kama kijikofia kudhihirisha Uislamu wao hali ya kuwa ndani ya mioyo yao wanaabudia muundo unaotumiwa kuumaliza Uislamu.

Ndio muundo (Umoja wa Mataifa) huo huo uliokaa nyuma na kutofanya lolote pale wanawake waja wazito wa Kiislamu walipotumbuliwa matumbo yao na Waserbia na kuwa ndio sababu ya vifo vyao. Ndio muundo huo huo uliosimama bila ya kuchukua hatua yoyote pale wanawake na watoto wadogo walipobakwa Kashmiri.
Muundo ambao ulisimama bila ya kusema lolote pale kina mama waliposhuhudia watoto wao wakiburuzwa usiku na majeshi na wasionekane tena kurudi. Kwa lipi? Kwa sababu wamesema kwamba wao ni wakimbizi ndani ya ardhi yao na ndio muundo huo huo ulioacha kusema kitu kwa wababe waliowatesa wanawake na watoto, kwa sababu hao wababe wanafuata mchezo wa Kimasoni. Kwa wale wanaochagua muundo huu wakadai wanampenda Allaah na Mtume Wake lakini wakichukia kile alichokileta, wakaachana na uongofu ambao ni Uislamu na wakajiegemeza na muundo wa kishetani wa Dajjaal, wakiishi maisha yao kwa mujibu wa kanuni zake na wakitarajia kutokana naye malipo ya kidunia, wakitupilia mbali ukweli ambao ni wa sheria za Allaah. Hao ndio wanaojikaribishia laana za Allaah.

Watangulizi wa Dajjaal wametengeneza muundo huu kuubomoa Uislamu aidha moja kwa moja kupitia jeshi na mabadiliko ya uchumi au kwa njia za kilaghai kwa kutumia dhana za fikra. Wamewagawa watu katika utaifa na ukabila ndani ya mioyo ya Ummah wa Kiislamu na kuteka ardhi na kuingiza maradhi. Woga wao mkubwa ni umoja wa Waislamu na kurudi upya ujumbe ulioletwa na Mtume wa mwisho kwa wanaadamu, na kila wanachofanya wanahakiksha wanazuia hili. Wamewaharibu Waislamu wakiwatengenezea muundo mwengine na kushajiiisha mgawanyo. Wameingiza lugha yao inayotumika dunia nzima na kuwalazimisha wote kujifunza au kutengwa na kupunguza Kiarabu kufikia hadhi ya chini ndani ya jamii na kinachowafanya kuwabakisha Waislamu si chengine isipokuwa mafuta.

Wakati wa kipindi cha Vita vya Kwanza vya Dunia, serikali za Kimasoni zilihakikisha kubomoa ukhalifa wa Kiislamu na mataifa yake. Sehemu inayoitwa Iraaq iliwekwa chini ya himaya ya Muingereza na mipaka inayoonekana sasa iliwekwa na wao na kupitia vita vya Iran na Iraaq. Baada ya uhuru wake, USA imekuwa na hamu ya kuitawala Iraaq kwa khofu ya kuja juu fikra safi za Kiislamu.

Vita vya Ghuba vimetimiza malengo mengi kuimarisha umoja wa Kimagharibi ili kuengeza migawanyiko miongoni mwa mataifa ya Kiislamu. Vimetumika kama ni sehemu ya majaribio ya zana zao za kivita na kemikali na madawa, lakini kubwa katika vita hivyo ilichofanikiwa ni kuhakikisha kuendelea kuwepo ngome kali ndani ya mashariki ya kati. Dajjaal ameweka ngome ya hakika ndani ya Uislamu wenyewe na kuhodhi vizuri ardhi takatifu za Waislamu. Lakini ingawa wanapanga, Allaah pia Anapanga na Allaah Ndie Mbora wa Wapangaji. Ushindi wa mwisho utakuwa ni kwa Waislamu. ALLAAHU AKBAR!

Hivyo ndugu zangu Waislamu, wanaume na wanawake, tuliposimama hapa sasa, hebu fikiria kidhati japo mara moja tu:


NEMBO KUU YA MAREKANI
Kwa mujibu wa Encyclopedia ya Encarta, Nembo Kuu ya Marekani inatambuliwa kama:
"Nembo Kuu ya Marekani na ambayo ni nembo rasmi ya Serikali ya Marekani ina pembe mbili, ikiwa na sehemu zote mbili za kwenda juu na kwenda chini. Na sehemu ya kwenda juu imekatwa kama ni die, lakini ubunifu wa kwenda chini umenakiliwa na unaonekana, kwa mfano, katika sarafu ya dola moja ya Marekani."

Umbo lililojitokeza zaidi katika sehemu ya juu ya nembo ni ndege wa Kimarekanieagle, akioneshwa akiwa na mbawa zilizotawanywa. Kifuani mwake kuna ngao yenye tepe 13 zilizosimama, 7 zikiwa ni nyeupe zinazopwesa na 6 nyekundu, zilizozungushiwa kwa utepe unaotoka mashariki kwenda magharibi wa rangi ya samawati (blue). Eagle huyo amekamata zaytuni katika ukucha wake wa kulia, kishada cha mishale 13 kushotoni, na mdomoni mwake kuna hati ndefu ya kuzungusha yenye maneno ya ujumbe mzito wa Kilatini: E pluribus unum ("Kutoka wengi, mmoja"). Kishada chenye nyota 13 zenye pembe tano, zikizungushiwa na urehemevu, unaonekana juu ya eagle.

Kuna jengo la mawe lenye pembe tatu, lililokatwa kidogo karibu na juu, kati kati kuna alama iliyokwenda chini kiupande pande.
Msingi wa jengo hilo limegandishwa na tarehe 1776 kwa tarakimu za Kirumi: MDCCLXXVI. Katika usawa wa kuashiria mbinguni, ndani ya kijengo cha pembe tatu kimezungukwa na urehemevu, likiwemo jicho moja linaloona la alama ya amri ya mungu. Juu ya jicho kumegandishwa ujumbe muhimu Annuit coeptis ("ametufurahia na matendo yetu"). Chini ya jengo hilo la pembe tatu kunaonekana ujumbe unaokwenda chini Novus ordo seclorum ("Mwenendo mpya wa wakati huu").

Nembo hii pia imegandishwa katika sarafu ya dola ya Marekani, ambayo chini yake imeandikwa: 'Novus Ordo Seclorum' yakifasiriwa kama: 'MWENENDO MPYA WA SIRI'.
Sasa jengo la pembe tatu lililobeba jicho moja juu yake linamaanisha nini? Mtume Muhamamd (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) miaka 1400 iliyopita, alitutahadharisha kuhusu Dajjaal katika maneno yafuatayo: Imesimuliwa na Ibn 'Umar, mara moja Mjumbe wa Allaah alisimama mbele ya watu, alimshukuru na alimhimidi Allaah kama Anavyostahiki na kisha kumtaja Dajjaal akisema:"Ninawahadharisha dhidi yenu (yaani Dajjaal) na hakuna Mtume yeyote (aliyekuja) isipokuwa amelihadharisha taifa lake dhidi yake. Hakuna shaka yoyote, Nuuh alihadharisha taifa lake dhidi yake, lakini ninawaambia kuhusiana naye kitu ambacho hakijapatapo kuzungumzwa na Mtume yeyote kwa taifa lake kabla yangu. Mutambue kwamba ana jicho moja, na Allaah Hana jicho-chongo." Hadiyth 4:553 (Swahiyh Al-Bukhaariy).


MAHEKALU YA KIMASONI
Kumekuwa na Mahekalu mengi ya Kimasoni yakifanyiwa ibada duniani kote. Hekalu la Kimasoni linaweza kuonekana kama ni jengo la mawe la pembe tatu (pyramid) au lenye alama za Kimasoni, kama utaliangalia vyema hekalu liliopo Islamabad (f-8/4), ubunifu wa hekalu hilo limekaa kama ni jengo la mawe la pembe tatu na lina alama za Kimasoni katika kuta zake.


MIPIRA YA SOKA
Kuliwahi kutengenezwa mpira na kuchapishwa bendera za nchi tofauti. Bendera ya Saudi Arabia ikiwa pia imechapishwa, bendera ambayo ina Tamko la Kiislamu (Kalimah ya Laa ilaaha illa Llaahu Muhammadun rasuulu Llaah). Innaa li Llaahi wa innaa ilayhi raaji'uun!

VIONGOZI WENGI NA WATU MAARUFU NI WAMASONI
"Hakuna shaka yoyote ndani ya akili yangu kwamba Wamasoni ndio waendeshaji wa Marekani."
Dave Thomas,
Muanzilishi wa Wendy's International.

"Kwangu mimi, Umasoni ni aina moja ya kujitolea kwa mungu na kuhudumia wanaadamu."
Norman Vincent Peale,
Waziri na Mwandishi.

"Umasoni ni ibada ya ustaarabu yenye sheria na mila bora na utashindana na aina yoyote ya mfumo wa mila na filosofia zilizopata kuwepo kwa (lengo la) kuipandisha juu hadhi ya mwanadamu."
Douglas MacArthur,
Mkuu wa Jeshi.

"Udugu wa Kimasoni ni miongoni mwa njia bora za kusaidia kubadili na kuhubiri jumuiya za watu, na sijapatapo kuliacha hilo tokea nilipokuwa mtoto, (Umasoni) umesimama pamoja nami katika miaka ya mishughuliko na miaka yenye kwenda kwa kasi."
George W. Truett,
Kiongozi wa Ubatizaji wa Kusini.

"Tunawakilisha udugu ambao unaamini uadilifu na ukweli na matendo ya heshima ndani ya jamii yetu… watu ambao wamefanya bidii ya kuwa ni wananchi bora… [na] kuitengeneza nchi bora kuwa bora zaidi. Hii ndio taasisi pekee duniani tunayoweza kukutana [katika] viwango tofauti vya watu wote wanaotaka kuishi sawasawa."
Harry S. Truman,
Raisi wa Marekani.

Viongozi wengi na watu maarufu na watu wenye kuheshimika wakiwemo wafanyabiashara, majeshi, wasomi, wanasiasa, na viongozi wa dini wamekuwa au wanaendelea kuwa Wamasoni.
[Picha hiyo ni ya sehemu ya kukutana Wamasoni nchini India – Grand Lodge of India]
Swami Vivekananda - Motilal Nehru - C. Rajagopalachari - Fakruddin Ali Ahmed - Omdat-ul-Omrah - P.C. Dutt - Eddy Arnold - Roy Acuff - Edwin E. "Buzz" Aldrin - Gene Autry - Daniel C. Beard - Francis J. Bellamy - Irving Berlin - Simon Bol¡var - Walter Boomer - Gutzon Borglum - Ernest Borgnine - Omar Bradley - James Buchanan - Arleigh Burke - Richard E. Byrd B. H. Carroll - Mark Clark - William Clark Dewitt Clinton - Ty Cobb - W. T. Connor - Jack Dempsey - James Doolittle - Arthur Conan Doyle - "Duke" Ellington - Henry Ford - Gerald Ford –


[Picha hapa chini ni sehemu ya kukutana kwa Wamasoni huko Bombay]
Benjamin Franklin - Clark Gable - James Garfield - Arthur Godfrey - Wolfgang von Goethe - Barry Goldwater - Samuel Gompers - John Hancock - Warren Harding - Jesse Helms - Sam Houston - Burl Ives - Andrew Jackson - Andrew Johnson - John Paul Jones - Benito Ju rez - Rudyard Kipling - Marquis de Lafayette - J. B. Lawrence - John Lejeune - Charles Lindbergh - John Marshall - George Marshall - Thurgood Marshall - Jos‚ Mart¡ - Charles Mayo - Douglas MacArthur - Abner McCall - William McKinley - James Monroe - Wolfgang Mozart - Louis D. Newton - Norman Vincent Peale - J. C. Penney - John Pershing - James Polk - Paul Revere - Herbert Reynolds - Roy Rogers - Will Rogers - Franklin D. Roosevelt - Theodore Roosevelt - Thomas S. Roy - L. R. Scarborough - Jean Sibelius - "Red" Skelton - John Phillip Sousa - William Howard Taft - Danny Thomas - Lowell Thomas - Strom Thurmond - George W. Truett - Harry S. Truman - Joseph Warren - John Wanamaker - George Washington - John Wayne.


{{Na (Mayahudi) walifanya hila; na Allaah Akazipundua hila zao; na Allaah Ndiye bora wa kupindua hila (za watu wabaya).}}
[3: 54]

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only