08-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa (Talaka Ya) Rejea

بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam

كِتَابُ اَلنِّكَاحِ
Kitabu cha Nikaah (Ndoa)

  بَابُ اَلرَّجْعَةِ
08-Mlango Wa (Talaka Ya) Rejea927.
عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ، {أَنَّهُ سُئِلَ عَنْ اَلرَّجُلِ يُطَلِّقُ، ثُمَّ يُرَاجِعُ، وَلَا يُشْهِدُ؟ فَقَالَ: أَشْهِدْ عَلَى طَلَاقِهَا، وَعَلَى رَجْعَتِهَا} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ هَكَذَا مَوْقُوفًا، وَسَنَدُهُ صَحِيحٌ
Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Aliulizwa kuhusu mtu aliyemtaliki mkewe kisha akamrejea wala hakushuhudisha mtu. Akasema: “Shuhudisha talaka yake na kumrejea kwake.”[1] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na ikiwa ni Mawquwf na Isnaad yake ni swahiyh]928.
وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، {أَنَّهُ لَمَّا طَلَّقَ اِمْرَأَتَهُ، قَالَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ، لِعُمَرَ: "مُرْهُ فَلْيُرَاجِعْهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْه
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Alipomtaliki mkewe, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia: “Muamrishe amrejee.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 
[1] Ina maana talaka na kumrejea mashahidi wawili ni lazima wawepo. Kama hakuna mashahidi, mwanaume au mwanamke anaweza kufanya kitu kwa kudanganya na ikasababisha matatizo zaidi. Kuita mashahidi ni lazima na ni jambo lenye kupendeza. Rai ya ‘Ulamaa wengi ni kuwa ni jambo linalopendeza kulifanya, lakini kwa ukweli haswa ni jambo la lazima.

0 Comments