09-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Ushirika Na Wakala


بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ
Kitabu Cha Biashara

بَابُ اَلشَّرِكَةِ وَالْوَكَالَةِ
09-Mlango Wa Ushirika[1] Na Uwakala[2]
742.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {قَالَ اَللَّهُ: أَنَا ثَالِثُ اَلشَّرِيكَيْنِ مَا لَمْ يَخُنْ أَحَدُهُمَا صَاحِبَهُ، فَإِذَا خَانَ خَرَجْتُ مِنْ بَيْنِهِمَا} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ 
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah amesema: Mimi ni wa Tatu wa washirika wawili madamu mmoja wao hajakhini mwenzake, atakapomkhini Nitatoka baina yao.”[3] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Al-Haakim]743.
وَعَنْ اَلسَّائِبِ بْنِ يَزِيدَ اَلْمَخْزُومِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّهُ كَانَ شَرِيكَ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَبْلَ اَلْبَعْثَةِ، فَجَاءَ يَوْمَ اَلْفَتْحِ، فَقَالَ: " مَرْحَباً بِأَخِي وَشَرِيكِي} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ مَاجَةَ 
Kutoka kwa As-Saaib bin Yaziyda Al-Makhzuwmiyy[4] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Yeye alikuwa ni mshirika wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kabla ya Unabii akamuambia: karibu ndugu yangu na mshirika wangu.”[5] [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na Ibn Maajah]744.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {اِشْتَرَكْتُ أَنَا وَعَمَّارٌ وَسَعْدٌ فِيمَا نُصِيبُ يَوْمَ بَدْرٍ..} اَلْحَدِيثَ. رَوَاهُ النَّسَائِيُّ وَغَيْرُهُ 
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilishirikiana mimi, ‘Ammaar na Sa’d katika tulichopata siku ya vita vya Badr.” Hadi mwisho wa Hadiyth [Imetolewa na An-Nasaaiy]745.
وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {قَالَ: أَرَدْتُ اَلْخُرُوجَ إِلَى خَيْبَرَ، فَأَتَيْتُ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فَقَالَ: "إِذَا أَتَيْتَ وَكِيلِي بِخَيْبَرَ، فَخُذْ مِنْهُ خَمْسَةَ عَشَرَ وَسْقًا} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nilitaka kuenda Khaybar nikamuendea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) nikamueleza akasema: Utakapomuendea wakala wangu Khaybar chukua wasaki (kapu) kumi na tano (tende) kutoka kwake.”[6] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha]746.
وَعَنْ عُرْوَةَ الْبَارِقِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  بَعَثَ مَعَهُ بِدِينَارٍ يَشْتَرِي لَهُ أُضْحِيَّةً..} اَلْحَدِيثَ. رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ فِي أَثْنَاءِ حَدِيثٍ، وَقَدْ تَقَدَّمَ 
Kutoka kwa ‘Urwah Al-Baariqiyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa dinari (moja) kununulia udhw-hiyyah.” Mpaka mwisho wa Hadiyth [Imetolewa na Al-Bukhaariy na imetangulia][7]747.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {بَعَثَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  عُمَرَ عَلَى اَلصَّدَقَةِ..} اَلْحَدِيثَ. مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtuma ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuchukua Zakaah.” Mpaka mwisho wa Hadiyth [Al-Bukhaariy, Muslim][8]748.
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  نَحَرَ ثَلَاثًا وَسِتِّينَ، وَأَمَرَ عَلِيًّا أَنْ يَذْبَحَ اَلْبَاقِيَ} اَلْحَدِيثَ. رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alichinja (ngamia) sitini na tatu akamuamrisha ‘Aliy[9] kuwachinja waliobakia (thelathini na saba).” Mpaka mwisho wa Hadiyth [Imetolewa na Muslim]749.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  فِي قِصَّةِ اَلْعَسِيفِ. قَالَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {وَاغْدُ يَا أُنَيْسُ عَلَى اِمْرَأَةِ هَذَا، فَإِنْ اِعْتَرَفَتْ فَارْجُمْهَا..} اَلْحَدِيثَ. مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema katika kisa cha muajiriwa kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ee Ubays nenda kwa mke wa bwana huyu, akikiri kosa umpige mawe…”[10] mpaka mwisho wa Hadiyth [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
[1] Ushirika ni muafaka baina ya washirika katika asili ya mali na faida. Katika Hadiyth hii kuna dalili kuswihi ushirika katika kuchuma na ushirika huu unaitwa ushirika wa kiwiliwili (Shirkat Al-Abdaan). Ushirika uko katika mafungu manne.

[2] Wakala ni kumpa mtu unaibu atakayekuwa badala yake katika majukumu yake kama vile kuuza, kununua na mfano wake.

[3] Hii ina maana kuwa ushirika wa mali na fedha ni jambo lililoruhusiwa, la kuzingatia ni uaminifu. Ushirika wenye uaminifu ndani yake huleta faida, uaminifu unapoondoka hasara huingia kwa washirika.

[4] Ibn Jawziy ametaja katika At-Taliqiyb jina lake lilikuwa As-Saaib bin ‘Aaidh Al-Makhzuwmiyy. Ibn ‘Abdil-Barr amesema alikuwa miongoni mwa Al-Muallafatul-Quluwb na aliposilimu alikuwa Muislamu mzuri. Ni Swahaba, aliishi hadi katika zama za ukhalifa wa Mu’aawiyah.

[5] Ushirika ulikuwepo hapo kabla na Uislamu ukauelekeza vizuri.

[6] Ina maana mtu anaweza kumuweka wakala wake katika mambo ya fedha. Kuna Hadiyth nyingine ambayo Jaabir anamuuliza Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amjibu nini mtu anayemtaka asimamie ukusanyi wa tende. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia aweke mkono katika mti wa mtende wa anayemuomba, wakati huo Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alishakuwa na wakala wake. Wasaki 15 ni kilo 2145.

[7] Tazama Hadiyth ya 686.

[8] Hadiyth inamalizikia hivi: Akaambiwa: “Ibn Jamiyl, Khaalid ibn Waliyd na Al ‘Abbaas ami yake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wamezuia (Zakaah). Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Ibn Jamiyl hawezi kukataa isipokuwa alikuwa fukara Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akamtajirisha. Ama Khaalid, nyinyi mnamdhulumu Khaalid. Hakika aliziweka zana zake za kivita katika njia ya Allaah. Ama Al-‘Abbaas Zakaah yake ninayo mimi na mfano wake.” Kisha akasema: Ee ‘Umar kwani hujui kuwa ami ya mtu ni mfano wa baba yake?” Katika Hadiyth hii muna dalili ya kiongozi kumwakilisha mtu kuchukua Zakaah.

[9] Ina maana kumpa wakala mtu achinje Udhwhiyya (mnyama) ni jambo linalokubalika kishariy’ah

[10] Hii ni dalili nyingine ya kuruhusu uwakala hata katika huduwd. Hadiyth hii ni dalili kuwa anayeamrishwa ni wakala wa kiongozi katika kutekeleza hadd (adhabu). Unays ni wakala katika kuhakiki madai ya zinaa, tena ni wakala katika kutekeleza adhabu.

0 Comments