12-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Kunyang’anya


بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ
Kitabu Cha Biashara

بَابُ اَلْغَصْبِ
12-Mlango Wa Kunyang’anya[1]
756.
وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  كَانَ عِنْدَ بَعْضِ نِسَائِهِ، فَأَرْسَلَتْ إِحْدَى أُمَّهَاتِ اَلْمُؤْمِنِينَ مَعَ خَادِمٍ لَهَا بِقَصْعَةٍ فِيهَا طَعَامٌ، فَكَسَرَتِ اَلْقَصْعَةَ، فَضَمَّهَا، وَجَعَلَ فِيهَا اَلطَّعَامَ. وَقَالَ: " كُلُوا " وَدَفَعَ اَلْقَصْعَةَ اَلصَّحِيحَةَ لِلرَّسُولِ، وَحَبَسَ اَلْمَكْسُورَةَ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ  .
وَاَلتِّرْمِذِيُّ، وَسَمَّى اَلضَّارِبَةَ عَائِشَةَ، وَزَادَ: فَقَالَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {طَعَامٌ بِطَعَامٍ، وَإِنَاءٌ بِإِنَاءٍ} وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa yuko kwa baadhi ya wakeze, mmoja wa Mama wa Waumini akamtuma mtumishi wake sahani yenye chakula akapiga ile sahani kwa mkono akavunja.[2] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akavikusanya vipande vile akaweka chakula ndani yake, akasema: Kuleni.[3] Akachukua sahani nzima akampa yule mtumishi, ile iliyovunjika akaizuia.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
Na At-Tirmidhiy akamtaja aliyepiga ni ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) na akaongeza: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Chakula kwa chakula na chombo kwa chombo.”[4] Ameisahihisa.757.
وَعَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ   {مَنْ زَرَعَ فِي أَرْضِ قَوْمٍ بِغَيْرِ إِذْنِهِمْ، فَلَيْسَ لَهُ مِنْ اَلزَّرْعِ شَيْءٌ، وَلَهُ نَفَقَتُهُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ.
وَيُقَالُ: إِنَّ اَلْبُخَارِيَّ ضَعَّفَهُ 
Kutoka kwa Raafi’ bin Khadiyj[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kulima katika ardhi ya watu bila ruhusa yao hana haki yoyote katika mazao, na gharama ni yake.”[6] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa An-Nasaaiy, na At-Tirmidhiy akasema ni Hassan]
Yasemekana kuwa Al-Bukhaariy ameidhoofisha758.
وَعَنْ عُرْوَةَ بْنِ اَلزُّبَيْرِ قَالَ: قَالَ رَجُلٌ مِنْ اَلصَّحَابَةِ، مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {إِنَّ رَجُلَيْنِ اِخْتَصَمَا إِلَى رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فِي أَرْضٍ، غَرَسَ أَحَدُهُمَا فِيهَا نَخْلًا، وَالْأَرْضُ لِلْآخَرِ، فَقَضَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  بِالْأَرْضِ لِصَاحِبِهَا، وَأَمَرَ صَاحِبَ اَلنَّخْلِ أَنْ يُخْرِجَ نَخْلَهُ. وَقَالَ: " لَيْسَ لِعِرْقٍ ظَالِمٍ حَقٌّ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَإِسْنَادُهُ حَسَنٌ 
وَآخِرُهُ عِنْدَ أَصْحَابِ " اَلسُّنَنِ " مِنْ رِوَايَةِ عُرْوَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ زَيْدٍ
وَاخْتُلِفَ فِي وَصْلِهِ وَإِرْسَالِهِ، وَفِي تَعْيِين صَحَابِيِّهِ 
Kutoka kwa ‘Urwah bin Az-Zubayr[7]  amesema: Mmoja wa Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alihadithia: “Watu wawili waligombana na kuenda kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika ardhi ambayo mmojawapo aliotesha mtende kuhusu ardhi ya mwingine. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akahukumu kuwa ardhi ni ya mwenyewe, akamuamrisha mwenye mtende kutoa mtende wake na akasema: “Mmea uliopanda kwa dhulma hauna haki.”[8] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Isnaad yake ni Hassan]
Mwisho wa Hadiyth inapatikana katika vitabu vya As-Sunan, kutoka kwa ‘Urwah naye kutoka kwa Sa’iyd bin Zayd. Hata hivyo wametofautiana ikiwa ni Mawsuwl (iliyounga) au ni Mursal (iliyoishia kwa Taabi’) kadhalika na jina Swahaba aliyesikia na kupokea kutoka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).759.
وَعَنْ أَبِي بَكْرَةَ، رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: فِي خُطْبَتِهِ يَوْمَ اَلنَّحْرِ بِمِنًى {إِنَّ دِمَاءَكُمْ وَأَمْوَالَكُمْ  وَأَعْرَاضَكُمْ عَلَيْكُمْ حَرَامٌ، كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا، فِي بَلَدِكُمْ هَذَا، فِي شَهْرِكُمْ هَذَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema katika khutbah yake ya siku ya Nahr alipokuwa Minaa alisema: “Hakika damu zenu na mali yenu ni haraam juu yenu kama uharamu wa siku yenu hii, katika mwezi wenu huu katika mji wenu huu.”[9] [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
[1] اَلْغَصْبِ (Al Ghaswb) ina maana ya kuchukua mali ya mtu kwa nguvu bila ridhaa yake.

[2] Alifanya hivyo kwa sababu ya wivu ikiwa wanawake wana wivu na waume wa kawaida.

[3] Akiwaambia wale aliokuwa nao.

[4] Kuna tofauti ya rai baina ya Wanazuoni, ikiwa kimeharibika au kuvunjika kwa aliyekiazima, itabidi alipe thamani yake au kukibadilisha na mfano wake. Hii inahusu vitu vinavyoweza kutiwa thamani tu. Ama vinginevyo lazima virudishwe vilivyo. Hadiyth hii inatilia mkazo vitu kurudishwa kama vilivyo.

[5] Raafi’ bin Khadiyj, Abuu ‘Abdillaah, Al-Khazraj Al-Answaariy. Ni mwenyeji wa Madiynah. Hakupigana katika vita vya Badr kwa sababu alikuwa na umri mdogo, lakini alihudhuria vita vya Uhud na vilivyofuatia. Alifariki mwaka wa 73 Hijriyyah.

[6] Ikitokezea mtu akalima shamba la mtu ya ruhusa ya mwenye shamba, hana haki ya mazao yake. Kikubwa anachoweza kudai ni gharama ya mbegu alizotia, na mazao yatakuwa ni ya mwenye kumiliki shamba.

[7] Huyu ni Abuu ‘Abdillaah ‘Urwah bin Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam bin Khuwayldi Al-Asad Al-Madaniy. Ni katika Mafuqahaa (Ulamaa wa Shariy’ah) saba wa Madiynah, na ni mmojawapo wa ‘Ulamaa wa kitabi’iyna. Alikuwa ni mtu madhubuti amepokea Hadiyth kutoka kwa baba yake, mama yake, Khalati yake ambaye ni ‘Aaishah Ummul-Mu-uminiyna (Mama wa Waumini), ‘Aliy, Muhammad bin Maslamah na Abuu Hurayrah. Ibn Sa’d amesema: “Ni madhubuti na ana Hadiyth nyingi, Faqihi, Mwanachuoni, thabiti, muaminiwa.” Alikuwa akisoma robo ya Qur-aan kila usiku (yaani juzuu saba na nusu). Alizaliwa mwanzoni mwa ukhalifa wa ‘Umar katika mwaka wa 23 Hijriyyah. Alifariki mwaka 94 Hijriyyah.

[8] Neno ظَالِمٍ (Dhwaalim) ni neno lenye maana mbaya sana, hapa ina maana ni mtu muovu, asiye na uadilifu. Hadiyth hii ni dalili kuwa anayetumia ardhi ya mwenyewe, ima kwa kupanda mimea, kujenga au kwa jambo lingine, anawajibika kutoa na kubomoa alichojenga, na gharama za kubomoa ni juu yake huyu mnyang’anyi. Lakini ile mimea na majengo ni mwenyewe (mwenye ardhi).

[9] Hadiyth hii imetajwa hapa kuwa kupora mali ya Muislam ni haraam. Na jambo hili limekubaliwa na Wanazuoni wote.

0 Comments