13-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Ash-Shuf’ah (Shufaa)بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ
Kitabu Cha Biashara

بَابُ اَلشُّفْعَةِ
13-Mlango Wa Ash-Shuf’ah (Shufaa)[1]

760.
عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {قَضَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ   بِالشُّفْعَةِ فِي كُلِّ مَا لَمْ يُقْسَمْ، فَإِذَا وَقَعَتِ اَلْحُدُودُ وَصُرِّفَتْ اَلطُّرُقُ فَلَا شُفْعَةَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ  .
وَفِي رِوَايَةِ مُسْلِمٍ: {اَلشُّفْعَةُ فِي كُلِّ شِرْكٍ: أَرْضٍ، أَوْ رَبْعٍ، أَوْ حَائِطٍ، لَا يَصْلُحُ أَنْ يَبِيعَ حَتَّى يَعْرِضَ عَلَى شَرِيكِهِ}
وَفِي رِوَايَةِ اَلطَّحَاوِيِّ: {قَضَى اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  بِالشُّفْعَةِ فِي كُلِّ شَيْءٍ} وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ 
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alihukumu shufaa katika kila mali isiyogawanywa. Itakapowekwa mipaka na njia zikabainishwa hakuna shufaa.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Shufaa katika kila ushirika, iwe ardhi, nyumba ya kuishi na bustani hairuhusiwi.” Katika tamshi linguine: “si halali (kuuza mshirika) mpaka amfahamishe mshirika mwenzake.”
Katika Riwaayah nyingine ya Atw-Twahaawiyy imesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amehukumu shufaa katika kila kitu.” Wapokezi wake ni madhubuti.761.
وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {جَارُ اَلدَّارِ أَحَقُّ بِالدَّارِ} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَلَهُ عِلَّةٌ 
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema “Jirani wa nyumba ana haki zaidi ya (kununua) nyumba.” [Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan lakini ina ila]762.
وَعَنْ أَبِي رَافِعٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {اَلْجَارُ أَحَقُّ بِصَقَبِهِ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ، وَفِيهِ قِصَّةٌ 
Kutoka kwa Abuu Raafi’ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jirani wa nyumba ana haki zaidi kwa nyumba.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy. Hadiyth hii ina kisa chake][2]763.
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {اَلْجَارُ أَحَقُّ بِشُفْعَةِ جَارِهِ، يُنْتَظَرُ بِهَا وَإِنْ كَانَ غَائِبًا إِذَا كَانَ طَرِيقُهُمَا وَاحِدًا} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ 
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jirani ana haki zaidi kwa shufaa ya jirani yake atamngojea hata kama hayuko iwapo njia yao ni moja.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) wapokezi wake ni madubuti (thiqah)]764.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {اَلشُّفْعَةُ كَحَلِّ اَلْعِقَالِ} رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ وَالْبَزَّارُ، وَزَادَ: "وَلَا شُفْعَةَ لِغَائِبٍ" وَإِسْنَادُهُ ضَعِيفٌ 
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Shufaa ni kama kufungua kamba (inayomzuia ngamia).”[3] [Imetolewa na Ibn Maajah na Al-Bazzaar akaongezea: “…wala hakuna shufaa kwa asiyekuwepo.” Na Isnaad yake ni dhaifu]
 
[1] اَلشُّفْعَةِ (Ash-Shuf’ah) shufaa ni mshirika kuchukua hisa ya mshirika mwenzake ambayo ameiuza kwa thamani yake aliyouzia nayo mshirika.
uzindushi: Kuna tofauti baina ya Ash-Shufa’ah (shufaa) na Ash-Shafaa’ah (shafaa) na Ash-shifaa’ah. Shufaa ni hii tuliyoieleza. Shafaa ni kuombea mtu msamaha. Shifaa ni poza.

[2] Kisa chenyewe ni hiki: kuwa Abuu Raafi’ akiwa pamoja na Miswaar bin Makhrama alimkabili Sa’d ibn Abii Waqaasw na kumuaridhia kumuuzia nyumba yake iliyokuwa jirani yake na nyumba ya Sa’d. Miswaar aliongea na Sa’d kuhusu jambo hilo. Sa’d alikubali kulipa Dinari mia nne (sarafu za dhahabu) kwa ajili ya nyumba ya Abuu Raafi’. Alikuwa tayari kulipa malipo ya mara moja au ya kidogo kidogo kama alivyotaka Abuu Raafi’. Aliposikia hivi Abuu Raafi’ akasema hakuuza nyumba hizi kwa fedha alizoahidiwa Dinari mia tano taslimu kwa sababu alimsikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema kuwa majirani wana haki zaidi kuliko wengine. Akasema vile vile lau angelisikia kabla asingeuza nyumba zake kwa bei ile.

[3] حَلِّ اَلْعِقَالِ (Hallil-‘Iqaal) ina maana muda tu magoti ya ngamia yatakapofunguliwa, wakati huo mara moja huamka. Hivyo hivyo, muda wa kuwa nyumba ishauzwa, au mtu ana haki kufahamu kuwa mwenzake anauza kitu naye asiharakishe mpaka ukapita muda mrefu basi hapo haki yake ya shufaa imeanguka. Na hii ndio maana ya msemo wa Hallil-‘Iqaal kawaida ya kufungua kamba hakuchukui muda mrefu.

0 Comments