21-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango wa Wasia


بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

بَابُ اَلْوَصَايَا
21-Mlango wa Wasia[1]


818.
عَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {مَا حَقُّ اِمْرِئٍ مُسْلِمٍ لَهُ شَيْءٌ يُرِيدُ أَنْ يُوصِيَ فِيهِ يَبِيتُ لَيْلَتَيْنِ إِلَّا وَوَصِيَّتُهُ مَكْتُوبَةٌ عِنْدَهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
 Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Haitakiwi kwa Muislamu iwapo ana jambo linalotakiwa kuusiwa, alale siku mbili ila awe ameshaandika wasia wake[2].”[3] [Al-Bukhaariy, Muslim]819.
وَعَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قُلْتُ: {يَا رَسُولَ اَللَّهِ! أَنَا ذُو مَالٍ، وَلَا يَرِثُنِي إِلَّا اِبْنَةٌ لِي وَاحِدَةٌ، أَفَأَتَصَدَّقُ بِثُلُثَيْ مَالِي؟ قَالَ: " لَا " قُلْتُ: أَفَأَتَصَدَّقُ بِشَطْرِهِ  ؟ قَالَ: " لَا " قُلْتُ: أَفَأَتَصَدَّقُ بِثُلُثِهِ ؟ قَالَ: " اَلثُّلُثُ، وَالثُّلُثُ كَثِيرٌ، إِنَّكَ أَنْ تَذَرَ وَرَثَتَكَ أَغْنِيَاءَ خَيْرٌ مِنْ أَنْ تَذَرَهُمْ عَالَةً يَتَكَفَّفُونَ اَلنَّاسَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 
Kutoka kwa Sa’d bin Abiy Waqqaasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuambia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Ee Rasuli wa Allaah! Mimi ni mwenye mali nyingi, wala hakuna atakayenirithi isipokuwa binti yangu mmoja tu. Je nitoe swadaqah thuluthi mbili za mali yangu? Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Hapana” nikasema: “Basi nitoe nusu yake?” akasema: “Hapana” Nikasema: “Je thuluthi (moja)? Akasema: “Thuluthi,[4] na hiyo thuluthi ni nyingi, kuwaacha warithi wako wakwasi, ni bora kuliko kuwaacha mafukara wakiomba watu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]820.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا أَنَّ رَجُلاً أَتَى اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنَّ أُمِّي اُفْتُلِتَتْ نَفْسُهَا وَلَمْ تُوصِ، وَأَظُنُّهَا لَوْ تَكَلَّمَتْ تَصَدَّقَتْ، أَفَلَهَا أَجْرٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ عَنْهَا؟ قَالَ: " نَعَمْ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ 
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa mtu mmoja[5] alimjia  Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mama yangu amekufa ghafla wala hakuusia na nadhani lau angelizungumza, angeliamuru itolewe swadaqah, je atapata ujira nikimtolea swadaqah? Akasema: “Ndio.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]821.
وَعَنْ أَبِي أُمَامَةَ اَلْبَاهِلِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  يَقُولُ: {إِنَّ اَللَّهَ قَدْ أَعْطَى كُلَّ ذِي حَقٍّ حَقَّهُ، فَلَا وَصِيَّةَ لِوَارِثٍ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ  إِلَّا النَّسَائِيَّ ، وَحَسَّنَهُ أَحْمَدُ وَاَلتِّرْمِذِيُّ ، وَقَوَّاهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ
 وَرَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، وَزَادَ فِي آخِرِهِ: {إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اَلْوَرَثَةُ} وَإِسْنَادُهُ حَسَنٌ
 Kutoka kwa Abuu Umaamah Al-Baahiliyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Kwa hakika Allaah Amempa kila mwenye haki haki yake, kwa hivyo hakuna wasia kwa mwenye kurithi.”[6] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa An-Nasaaiy, Ahmad na At-Tirmidhiy wamesema ni Hasan, Ibn Khuzaymah na Ibn Al-Jaaruwd wameipa nguvu]
Pia Ad-Daaraqutwniyy ameipokea kutoka katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) mwisho wake akaongeza: “…isipokuwa watakapopenda wanaorithi.” [Isnaad yake ni Hassan]822.
وَعَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ اَلنَّبِيُّ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {إِنَّ اَللَّهَ تَصَدَّقَ عَلَيْكُمْ بِثُلُثِ أَمْوَالِكُمْ عِنْدَ وَفَاتِكُمْ، زِيَادَةً فِي حَسَنَاتِكُمْ} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ 
 وَأَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَالْبَزَّارُ مِنْ حَدِيثِ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ
وَابْنُ مَاجَهْ: مِنْ حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ  وَكُلُّهَا ضَعِيفَةٌ، لَكِنْ قَدْ يَقْوَى بَعْضُهَا بِبَعْضٍ. وَاَللَّهُ أَعْلَمُ
Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kwa hakika Allaah Amekupeni swadaqah[7] theluthi ya mali yenu mtoe wakati wa kufa kwenu ili kuzidisha mema yenu.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy]
Ahmad na Al-Bazzaar wameipokea kutoka katika Hadiyth ya Abuu Ad-Dardaa.
Na Ibn Maajah ameipokea kutoka katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah. Mapokezi yote ni dhaifu. Hata hivyo zimetiliana nguvu zenyewe na zikawa ni Hasan. Allaah ni Mjuzi. 

 
[1] Kilugha Waswiyyah (wasia) ina maana ya kuagiza, kushauri, kupendekeza kitu. Kulingana na Shariy’ah ni wasia anaoacha (kwa theluthi moja) ya mali ya marehemu kutumika baada ya kifo chake.

[2] Kabla ya kuteremka kwa Aayah ya mirathi, kuweka wasia ilikuwa ni wajibu. Hata hivyo baada ya Wahyi huu amri hii ilibatilishwa. Hata hivyo inawezekana mtu akaweka wasia katika yasiyokuwa mambo ya kurithi. Leo hii, suala hili limekuwa muhimu sana, kwa mfano kwa mtu kuwepo na mtoto wake pamoja nae kuweka wasia kwa ajili ya mjukuu wa mtoto wa aliyefariki. Uandishi wa wasia sio muhimu. Hata hivyo ni muhimu kuthibitisha wasia uliotamkwa, ili kuzuia sintofahamu yoyote inayoweza kujitokeza huko mbeleni.

[3] Katika Riwaayah nyingine ya Muslim imesema: “Awe atalala masiku matatu.” Ibn ‘Umar amesema: “Tangu nimsikie Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema maneno hayo sijapitiwa na usiku ila wasia wangu uko kwangu.”

[4] Wasia unaweza kuweka kwa thamani ya juu zaidi isizidi theluthi moja tu kwa mali yote mtu anayomiliki. Ikiwa ni chini ya theluthi ni bora. Hata hivyo kwa niaba ya warithi wengine anaweza kuusia zaidi ya theluthi moja ikiwa warithi wenyewe wako hai, vinginevyo hairuhusiwi kuusia zaidi ya theluthi moja.

[5] Mtu huyu alikuwa ni Sa’d bin ‘Ubaadah. Tunajifunza katika Hadiyth hii kuwa watoto wa kike na wa kiume wanaorithi wanaweza kutoa swadaqah katika mali ya mirathi bila ya wasia wa hilo.

[6] Hii ina maana wasia hauwekwi kwa wanaorithi, lakini kwa ruhusa ya warithi wengine, inaruhusiwa, kama ilivyo kuweka wasia wa zaidi ya theluthi moja inaruhusiwa kwa mtu yeyote kwa ruhusa ya warithi wengine.

[7] Katika lugha ya kiarabu neno Ihsaan ni kupendezesha, mtu akiwa hai mwenye nguvu anatumia mali na utajiri wake autakavyo, baada ya kufa kwake hana mamlaka na mali aliyoacha. Hapa ndipo Allaah Akamtaka mtu kuweka wasia wa theluthi ya mali yake kabla ya kufa kwake ili imuongezee katika amali yake.

0 Comments