01-Imaam Bin Baaz: Kuongeza Rakaah Moja Baada Ya Imaam Kumaliza Witr

Kuongeza Rakaah Moja Baada Ya Imaam Kumaliza Witr

Imaam Bin Baaz (Rahimahu-Allaah)SWALI:

Kuna watu wengine wanaposwali Witr na Imaam na anapotoa salaam wanainuka na kuswali Raka'ah moja nyingine, kwa sababu wanataka kuswali zaidi kabla ya kuswali Witr baadaye usiku.  Nini hukumu ya kufanya hivi?  Je, Inahesabika kuwa amekwenda kinyume na Swalah pamoja na Imaam?


JIBU:

Hatuoni ubaya wowote kufanya hivyo, na ‘Ulamaa wamesema pia hakuna ubaya kufanya hivyo ili Swalaah yake ya Witr iwe ndiyo Swalaah ya mwisho usiku.  Atahesabika kuwa ameswali na Imaam mpaka kamaliza kwa sababu amekaa naye hadi kamaliza kisha ndio kaongeza Raka'ah moja kwa sababu inayokubalika katika Shariy’ah ili apate kuswali tena baadaye usiku. Wala haimaanishi kwamba hakubakia na Imaam mpaka mwisho lakini hakumaliza tu naye na kaichelewesha kidogo.


[Imaam ‘Abdul-‘Aziyz bin Baaz -Al-Jawaab As-Swahiyh min Ahkaam Swalaat Al-Layl Wat-Taraawiyh -  Uk. 41]

0 Comments