02-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kushika Msahafu Katika Swalaah Ya Taraawiyh Kumfuatilizia Imaam

Kushika Mswahafu Katika Swalaah Ya Taraawiyh Kumfuatilizia Imaam

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)SWALI:

Nini hukumu ya kukamata Msahafu ili kumfuatiliza Imaam anayewalisha Swalah ya Taraawiyh katika Ramadhaan?


JIBU:

1. Kushika Msahafu ni kinyume na Sunnah kwa sababu nyingi:

2. Inamzuia mtu kuweza kuweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto

3. Inasababisha harakati nyingi kama kufungua Msahafu, kufunga na kuuweka chini ya kwapa.

4. Harakati  hizo zinawashawishi wanaoswali naye.

5. Inamzuia mwenye kuswali kutazama sehemu ya kusujudu. 'Ulamaa wengi wameona na kusema kuwa kutazama sehemu ya kusujudu ni Sunnah na bora.

6. Anayefanya hivyo (kushika Msahafu) huenda akasahau kama yuko katika Swalah isipokuwa ikiwa moyo wake umenyenyekea katika Swalah, kwani bila ya kushika Msahafu, kusimama kwake kunakuwa kwa unyenyekevu kutokana na kuweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto, akiinamisha kichwa chake kutazama sehemu ya kusujudu. Hivi humsababisha kumkumbusha kuwa yuko katika Swalah na yuko na Imaam.


[Gazeti la Da'awah Nambari 1771 – Ukurasa 45]

0 Comments