03-Imaam Al-Albaaniy: Imaam Kutoa Mawaidha Baina Ya Swalaah Za Taraawiyh

Imaam Kutoa Mawaidha Baina Ya Swalaah Za Taraawiyh

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu-Allaah)SWALI:

Je, inajuzu kwa Imaam wa Masjid ambaye anaswalisha watu katika Tarawiyh kuwakumbusha watu wakati wa mapumziko na kuzungumzia juu ya Swalaah na juu ya kumfuata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwaonya baadhi ya watu wa bid’ah na washirkina?


JIBU:

Yote ni sawa.

Ikiwa kama ni tukio limetokea, ni waajib kufanya hivyo.
Ikiwa ni ada (Imaam) kuonya watu kila baada Raka’ah na mfano wake, hii ni kinyume na Manhaj ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).


[Silsilatul-Hudaa Wan-Nuwr (656)]

0 Comments