03-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Hukmu Ya Kujimai Mchana Wa Ramadhwaan

Hukmu Ya Kujimai Mchana Wa Ramadhwaan

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)SWALI:

Nini hukmu ya aliyejimai (kitendo cha ndoa) na mkewe mchana wa Ramadhwaan?


JIBU:

Ikiwa wote walikuwa wako katika udhuru wa kutokuwa katika swawm; mfano kama walikuwa safarini, hakuna ubaya hivi hata kama wote walikuwa katika swawm. Lakini ikiwa walikuwa katika hali ya kuwajibika swawm, basi ni haraam kwao wote na wanatakiwa walipe siku hiyo, na juu yake kafara nayo ni kuachia huru mtumwa, na kama hawawezi basi wafunge miezi miwili mfululizo (bila ya kukatiza), na ikiwa hawawezi kufanya hivi basi walishe masikini sitini  au watu wanaohitaji. 

Kufanya hivyo inawapasa wote wawili kila mmoja afanye sehemu yake. Lakini kama mke alilazimishwa kufanya kitendo hicho basi yeye haimpasi kulipa kafara.


[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Fataawa Ramadhwaan – Mjalada 2, Ukurasa 606, Fatwa Namba 597 - Fataawa Imaam Ibn 'Uthaymiyn –Mjalada 1, Ukurasa  541-542]

0 Comments