08-Shaykh Swaalih Al-Fawzaan: Kuswali Taraawiyh Nyumbani Ni Bora Au Kuiswali Msikitini?

Kuswali Taraawiyh Nyumbani Ni Bora Au Kuiswali Msikitini?

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaahu)SWALI:

Kuna miongoni mwa Twulaabul-'Ilm anasema kuwa kuiswali Swalaah ya Taraawiyh nyumbani ni bora zaidi kuliko kuiswali Msikitini. Akitolea ushahidi Hadiyth isemayo, "Swalaah ya Naafilah nyumbani ni bora kuliko Msikitini kwa daraja ishirini na tano. Anasema kuwa Swalaah ya Taraawiyh ni Naafilah na ndio kauli ya Imaam Maalik. Hili ndilo analolieleza wanafunzi. Je, yepi maoni yako?


JIBU:

Hili ni kosa.

Hili ni kosa kubwa, linakwenda kinyume na uongofu wa Salafus-Swaalih.

(Salafus-Swaalih) Walikuwa wakikusanyika Misikitini wakiswali Taraawiyh. Taraawiyh ni nembo iliyo dhahiri katika Shariy´ah za Dini. Iswaliwe Msikitini.

Kuiswali Msikitini ni bora kuliko kuiswali nyumbani. Hata kama kuiswali nyumbani inajuzu, lakini kuiswali Misikitini na kudhihirisha nembo hii na kuwa pamoja na Waislamu ni bora.

0 Comments