Imaam Ibn Taymiyyah: Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Upungufuu Katika Akili Na Dini

Amesema Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu-Allaah):   

Kutamka niyyah ni upungufu katika akili na  Dini. 
Ama katika Dini kwa sababu ni bid’ah, na katika akili ni kwa sababu ni sawa na ambaye anataka kula chakula husema: “Nanuia kuweka mkono wangu katika chombo hiki kwa kutaka nichote humo tonge la chakula niweke mdomoni mwangu kisha nimeze ili nishibe.”
Basi huu ni ujinga na upumbavu.


[Al-Fataawaa Al-Kubraa (2/213)]

0 Comments