Majuto Ya Nafsi - 2

Nafsi ikiendelea kujuta kutamani kuwa ingelipata uongofu.


}}أَوْ تَقُولَ لَوْ أَنَّ اللَّهَ هَدَانِي لَكُنتُ مِنَ الْمُتَّقِينَ{{

{{Au iseme (nafsi): “Lau Allaah Angeliniongoa, bila shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye taqwa.”}}[Az-Zumar: 57
].

Nafsi hiyo inapofikishwa na Mola wake kuonyeshwa maandalio yake kama ni jazaa yake kutokumtii alipokuwa duniani, yaani adhabu ya Moto wa Jahannam, hutamani kama angelipewa fursa arudi kufanya mema lakini wapi! Tayari keshachelewa!

 }}أ وْ تَقُولَ حِينَ تَرَى الْعَذَابَ لَوْ أَنَّ لِي كَرَّةً فَأَكُونَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ{{

{{Au iseme pale itakapoiona adhabu: “Lau ningelikuwa na (fursa ya) marejeo (ya kurudi duniani) basi ningekuwa miongoni mwa watendao wema.”}} [Az-Zumar: 58]

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ametuelezea hali ya majuto hayo yatakavyokuwa kwa kutupa picha ya watu wa Motoni watakavyotamani makazi ya watu wa peponi, na watu wa peponi watakavyoona makazi ya watu wa Motoni   katika Hadiyth ifuatayo:

‏((‏عن ‏ ‏أبي هريرة رضي الله عنه  ‏ ‏قال: ‏قال رسول الله ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم: ‏ ‏كل أهل النار يرىمقعده من الجنة فيقول لو أن الله هداني فتكون عليه حسرة قال: وكل أهل الجنة يرى مقعده منالنار فيقول لولا أن الله هداني قال: فيكون له شكرا )) إمام أحمد
((Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه   ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema; Kila mtu wa Motoni ataona makazi yake (aliyoandaliwa) peponi atasema; “Laiti Kama Allaah Angelinihidi,” kisha huwa majuto kwake. Akasema; Na kila mtu wa Peponi ataona makazi yake ya Motoni atasema; “Kama ingelikuwa si Allaah kunihidi.” Akasema; kisha itakuwa sababu ya kushukuru kwake.)) [Imaam Ahmad].


Na kama tunavyojua kuwa maisha ya Aakhirah ndio maisha ya milele, na haya ya dunia ni starehe ndogo tu. Kama Anavyosema Allaahسبحانه وتعالى :

}}وَمَا هَذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ{{

{{Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na nyumba ya Akhera ndiyo maisha khasa; laiti wangeli kuwa wanajua!}}[Al-‘Ankabuut: 64
].

Nayo nyumba hiyo ya Aakhirah ni ya wale wamchao Allaah tu, wenye kufanya vitendo vyema vyenye kumridhisha Mola wao. 

}}وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَلَلدَّارُ الآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ أَفَلاَ تَعْقِلُون{{

{{Na maisha ya dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao. Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wenye taqwa. Je, basi hamtumii akili?}} [Al-An’aam: 32
].

Lakini waovu wote hawatopata neema ya hiyo nyumba bora ya Aakhirah, bali malipo yaoyatakuwa ni makazi mabaya na hali wakiwa na majuto, baada ya kutambua kuwa wako katika khasara kubwa za nafsi zao pamoja na za jamaa zao:

}}قُلْ إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَلَا ذَلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ{{

{{Sema: “Hakika waliokhasirika ni wale waliokhasiri nafsi zao na ahli zao Siku ya Qiyaamah. Tanabahi! Huko ndiko kukhasirika dhahiri.”
}} [Az-Zumar: 15
].


**********

0 Comments