Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 4

Suala Nambari 4 Linaloeleweka Vibaya

Uislamu unakubaliana zaidi na Waarabu tu kwa sababu:
·                     Waislamu wengi ni Waarabu
·                     Qur-aan ipo kwa Kiarabu

JIBU
Hoja ya mwanzo kuhusu suala hili linaloeleweka vibaya ipo mbali na ukweli. Waislamu walio zaidi ya bilioni moja duniani, basi kati ya asilimia 18 tu ni Waarabu. Nchi zilizo na idadi kubwa ya Waislamu duniani ni Indonesia. Nchi ya pili yenye idadi kubwa ya Waislamu ni Bangladesh. Sio nchi hata moja kati ya hizi ni ya Kiarabu.

Uislamu ni dini yenye kukua kwa kasi duniani (Encyclopedia Britannica). Ina wafuasi kwenye mabara yote yenye idadi kubwa ya watu, na pia inakubalika kwa Waarabu na wasio Waarabu. Waislamu hadi itakapofikia mwisho mwa karne, wanatarajiwa kuwa ni dini kubwa kabisa kati ya dini zenye wafuasi wachache largest religious minority nchini Marekani, wakiwashinda Mayahudi.

Lalamiko la ulimwengu la Uislamu kwa Waarabu na wasiokuwa Waarabu linafuatia ingawa Qur-aan ni ya Kiarabu. Allaah Anaelezea ndani ya Qur-aan kwamba njia hii ya maisha inayoitwa Uislamu ni ya watu wote (tafsiri inafuata):
{{Nasi Hatukukutuma, (Hatukukuleta) ila uwe rehema kwa walimwengu (wote).}} [21:107]

{{Na Hatukukutuma (Hatukukuleta) ila kwa watu wote, uwe Mtoaji wa habari nzuri na Muonyaji; lakini watu wengi hawajui (lolote, wanajifuatia tu waliyowakuta nayo wazee wao).}} [34:28]

Juu ya hivyo, Muumba Hatumii kigezo cha rangi au lugha ya mama mother tongue kuwahukumu, wawe ni Waarabu au sio. Badala yake, ni kiwango cha kumtambua Allaah ndicho kigezo.

{{Enyi watu! Kwa hakika Tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja; Aadam) na (yule yule) mwanamke (mmoja; Hawwaa). Na Tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi; siyo mkejeliane). Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Allaah zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote).}} [49:13]

Uchaguzi wa Kiarabu kuwa ni lugha ya Qur-aan umeelezwa kiurahisi na kiuwazi (tafsiri inafuata):
{{Na lau kama Tungaliifanya Qur-aan kwa lugha isiyo ya Kiarabu wangalisema: “Kwa nini Aayah zake hazikupambanuliwa? Lo! Lugha isiyokuwa ya Kiarabu na (Mtume) Mwarabu! (Mambo gani haya)!” Sema: “Hii (Qur-aan) ni uongofu na poza kwa wale walioamini; na wale wasioamini umo uzito katika masikio yao; na hiyo (Qur-aan) ni giza kwao. (Hawasikii. Kama kwamba) hao wanaitwa, na hali ya kuwa wako mbali kabisa.}} [41:44]

Hata hivyo, ni muhimu pia kutilia mkazo kwamba Qur-aan ikiwa na uteremsho wa mtindo wa Kiarabu ni Neno sanifu la Muumba, lakini tafsiri yoyote sio (Qur-aan). Kila tafsiri kiusahihi inaitwa kuwa ni tafsiri na fafanuzi, kwani kila mfasiri anaingiza matashi/ upendeleo (bias) wake.

Itaendelea in Shaa Allaah....

0 Comments