Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 29

Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا  وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni walio bora kwa wake zao kwa tabia))  [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]Mafunzo na Mwongozo:


1. Uislamu unasisitiza kuwa na tabia njema kwa kila mtu.2. Mume anasisitizwa kumfanyia wema mkewe katika maisha ya ndoa, si kumfanyia uovu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):


وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ   
  Na wala msisahau fadhila baina yenu.  [Al-Baqarah (2: 237)]

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):


  وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ  
Na kaeni nao kwa wema. [An-Nisaa (4: 19)]


Pia rejea kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): [Ar-Ruwm 30: 21]


3. Inapasa kuweko subira baina ya mume na mke katika mitihani inayowakabili ya maisha baina yao. [((Na mkisubiri ni kheri kwenu)) [An-Nisaa (4: 25)].4. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kigezo bora kabisa katika kuamiliana na wake [Al-Ahzaab (33: 21)].

Pia Hadiyth zifuatazo:


 ((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli])) [Ibn Maajah na Ad-Daarimiy].


((Mwanamke ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea kupinda, nakuusieni [kuwafanyia wema]) wake zenu)) [Al-Bukhaariy, Muslim]


((Allaah, Allaah, kwa wanawake,  hao ni wasaidizi wenu walio kwenye mikono yenu, mmewachukuwa kama ni amana kutoka kwa Allaah, na imekuwa halali tupu zao kwenu kwa neno lake Allaah  [iyjaab na qubuwl])) [Muslim, Abu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]

Rejea pia Hadiyth namba (28), (35), (40).

0 Comments