Hatua za mwanasiasa mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi

Geert Wilders, Mwanasiasa mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi sambamba na kutoa mwaliko, ametaka kufanyika mashindano ya vibonzo vya kumdhalilisha Mtume Muhammad (saw) kwa lengo la kujeruhi hisia za Waislamu.
Wilders ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akitaka kufanyika mashindano hayo ya vibonzo kumhusu Mtume wa Uislamu (saw). Mwaka jana mwanasiasa huyo mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi na kutokana na mashinikizo yaliyotokana na malalamiko ya kupinga mashindano ya vibonzo vyenye kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) alilazimika kulegeza msimamo na kuvunja mashindano hayo.
Katika ujumbe huo kwenye mtandao wa Twitter Geert Wilders amewakata watu wamtumie vibonzo vyao, hata hivyo saa chache baada ya kutumwa, ujumbe huo umefutwa bila kutajwa sababu ya kufutwa kwake. Mwaka 2005 gazeti la Kiholanzi la Jyllands-Posten lilisambaza vibonzo vyenye kumvunjia heshima Nabii Muhammad (saw) suala lililoibua maandamano makubwa ya kulaani kitendo hicho kote duniani. Hatua na mienendo ya kibaguzi dhidi ya Uislamu ya wanasiasa na vyama vya kibaguzi barani Ulaya, imekuwa ikijiri mbele ya kimya cha serikali za madola ya Ulaya. 

0 Comments