Jinsi ya kupika Malfuuf (Mviringisho) Wa Wali Na Nyama Katika Kabeji

Vipimo:
Kabeji - 1
Mchele - 1 kikombe
Nyama ya kusaga - 1/4 Pound
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Kitunguu - 1
Parsely - 1 msongo (bunch)
Nyanya - 1
Garama Masala (au bizari mchanganyiko) - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi

Vifaa Vya Kutia Katika Kupika Malfuuf: 
Kidonge cha supu (Stock cube) -  1
Samli au mafuta - 1 kijiko cha supu
Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha chai
Nyanya kata ndogo ndogo - 1


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
 1. Chambua majani ya kabeji moja moja yasikatike.
 2. Chemsha maji tia chumvi kidogo, kisha tia majani ya kabeji kwa dakika moja yalainike. Epua, chuja na weka kando katika sinia.
 3. Osha mchele, urowanishe muda kidogo.
 4. Katakata kitunguu, nyanya na parsely ndogo ndogo.
 5. Changanya nyama na thomu, tangawizi, pilipili, kitunguu, nyanya, parsely, bizari na chumvi. 
 6. Kisha changanya pamoja na mchele ikiwa tayari kwa kujazia katika kabeji.
 7. Tandaza jani la kabeji kisha utie mchanganyiko uliotayarisha na uviringishe. Tazama picha.
 1. Panga kabeji zote katika sufuria kisha utie maji kiasi yasifikie kufunika kabeji.
 2. Tia kidonge cha supu, samli, nyanya uliyokata ndogo ndogo na nyanya kopo.
 3. Funika upike moto mdogo mdogo hadi maji yakaribie kukauka.
 4. Epua, na panga kabeji katika sahani zikiwa tayari kuliwa.

0 Comments