Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 5

Suala Nambari 5 Linaloeleweka Vibaya


Uislamu unamkataa Yesu kwa sababu:
·                     Yesu hakubaliki kuwa ni ‘mtoto wa Mungu’

JIBU:
Zote mbili; Qur-aan na Sunnah zinatufundisha kwa msisitizo na bila ya wasiwasi kwamba Muumba Anatambua tamko la Utatu kuwa ni uongo ulio mkubwa mno. Qur-aan inaeleza (iliyotafsiriwa):
{{Na (makafiri) husema: “(Allaah) Mwingi wa rehema amejifanyia mtoto. Bila shaka mumeleta jambo lichukizalo kabisa (kwa kusema hivyo). Zinakaribia mbingu kutatuka kwa (tamko) hilo na ardhi kupasuka na milima kuanguka (ikakatika) vipandevipande. Kwa kule kudai kuwa (Allaah) Mwingi wa rehema ana mtoto. Wala haiwi kwa (Allaah), Mwingi wa rehema kuwa ana mtoto. Hakuna yoyote aliyomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa (Allaah), Mwingi wa rehema hali ya kuwa ni mtumwa (Wake).}} [19:88-93]]

Hata hivyo, suala hilo linaloeleweka vibaya haliendani na hoja zinazotolewa hapo juu kwamba Yesu (‘Iysaa) anakataliwa (moja kwa moja). Ni vyema kutanabahisha kwa kusema kwamba inakataliwa kumueleza Yesu (‘Iysaa) kama ni ‘mtoto wa Mungu’. Kwa kuwa ni Mtume wa Allaah, Yesu anatunukiwa cheo chake cha heshima namna walivyopewa Mitume wote, kama ambavyo Aayah ifuatayo inavyotamka (tafsiri):
{{Semeni nyinyi (Waislamu waambiwe Mayahudi na Manaswara; waambieni): “Tumemwamini Allaah na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’aquub na kizazi (chake Ya’aquub); na waliyopewa Muusa na ‘Iysaa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutafautishi baina ya yoyote katika hao. (Wote tunawaamini); na sisi tumenyenyekea Kwake.}} [2:136]

Itaendelea In Shaa Allaah...

0 Comments