Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 6

Uislamu unaamrisha kumuabudia mwanaadamu kwa sababu:
·                     Waislamu ni ‘Wafuasi wa Muhammad’

JIBU:
Wasio kuwa Waislamu wa kale ambao walionekana kama kwamba ni watafiti wa Uislamu waliita ‘Dini ya Muhamaadi’, wakimaanisha kwa maana nyengine kwamba Waislamu walimuabudia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo, msingi wa suala hili (la uongo) ni kwamba hakika linatokana na wasiokuwa Waislamu. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa hapo juu, ‘Muislamu’ ni “yule anayemnyenyekea Allaah”. Asili ya Uislamu ni kwenye hali ya umoja ulio safi, tena safi, safi kabisa. Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{Sema: Yeye ni Allaah ni Mmoja (tu). Allaah (tu) Ndiye anayestahiki kukusudiwa (na viumbe Vyake vyote kwa kumuabudu na kumuomba na kumtegemea). Hakuzaa wala Hakuzaliwa. Wala hana anayefanana Naye hata mmoja.}} [112:1-4]

{{Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume tu. Wamepita kabla yake Mitume (wengi kabisa). Akifa au akiuawa ndiyo mtarudi nyuma (kwa visigino vyenu), muwe makafiri kama zamani? Na atakayerudi nyuma kwa visigino vyake hatamdhuru Allaah chochote. Na Allaah Atawalipa wanaomshukuru.}} [3:144]

Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah katika Swahiyh al-Bukhaariy, tunaona:
Amesimulia Mu’aadh bin Jabal: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ewe Mu’aadh! Je unatambua haki ya Allaah juu ya waja Wake?” Nikasema: “Allaah na Mtume Wake wanajua lililo bora” Mtume akasema: “Kumuabudia Yeye (Allaah) Pekee na bila ya kumshirikisha na chochote pamoja Naye (Allaah) kwenye ibada. Je unatambuwa haki yao juu Yake?” Nikajibu: “Allaah na Mtume Wake wanajua lililo bora” Mtume akasema: “Kutowaadhibu (kama wakimuabudu).” [9:93:470]

Amesimulia ‘Umar: Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Musivuke mpaka katika kunisifu kama Wakristo walivyomsifu mtoto wa Maryam, kwani mimi ni mja. Hivyo, niiteni Mja wa Allaah na Mjumbe Wake.” [4:55:654]

Itaendelea In Shaa Allaah...

0 Comments