Muislamu wa kwanza kuishi nchini Marekani: Anthony the Turk

Hati ya mwaka 1643 iliyopatikana hivi karibuni imesaidia kutoa mwanga juu ya Muislamu wa kwanza kuishi nchini Marekani

Nyaraka iliyogunduliwa hivi karibuni inaonesha kwamba muislamu wa kwanza kuingia nchini Marekani ni Anthony Jansen Van Salee ambaye aliingia jijini New York mwaka 1630.
Katika mauzo yaliyofanywa na makumbusho maarufu New York ijulikanayo kama “Christie museum” ilikuwepo hati ya karne ya 17 iliyokuwa na maelezo yanayohusiana na Van Salee. Hati hiyo ilinunuliwa na shirika la historia la Brooklyn kwa thamani ya dola elfu 27 na 500.
Julie Golie, Kiongozi wa ukusanyaji nyaraka wa taasisi alisema
“Tunafahamu kwamba Muislamu wa kwanza kuja New York yumkini alitokea Afrika kutokana na biashara ya utumwa lakini hati ya mwaka 1643niliyopatikana hivi sasa ni mfano wa kwanza unaoonyesha muislamu aliyeishi akiwahuru na mpaka kufikia  kumiliki ardhi nchini humo. Hatuna uhakika ni kwa kiasi gani Anthony Jansen Van Salee alikuwa akijitambulisha kwa utambulisho wa Uislamu lakini kitabu chake cha Quran kilichouzwa katika mnada mwanzoni mwa karne ya 20, kinaweza kutoa mwanga wa historia na utambulisho wake.”
Taasisi ya Uholanzi “New Netherland Institute” ilifanya utafiti kuhusu watu wenye asili ya Uholanzi waliokuwa wakiishi New York kipindi hicho wakati jiji hilo likitawaliwa na Uholanzi na likijulikana kama  “New Amsterdam’’. Golie aliyesema Jina la Van Salee lilipatika mara kwa mara katika nyaraka za kihistoria, aliongeza kwamba:
“Rekodi za kimahakama zinaonyesha Van Salee alijulikana pia kwa jina la 'Anthony the Turk' lakini katika kipindi hicho kwa ujumla waislamu walikuwa wakiitwa 'Türk'”

0 Comments