01-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Kwa nini Allaah Katuumba?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu
Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.
Imetarjumiwa na: Muislamublog.com


01-Kwa nini Allaah Katuumba?

Allaah Ametuumba ili tumuabudu na tusimshirikishe Naye kwa chochote.
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾
Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. [Adh-Dhaariyaat: 56]

((حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ أَنْيَعْبُدُوهُ، وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا))متّفق عَلَيهِ
((Haki ya Allaah kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

0 Comments