03-Swalaah – Kuwajibika Na Fadhila Zake: Amri za Mwanzo Kwa Manabii Waliopita

Swalaah – Kuwajibika Na Fadhila Zake

03- Amri Za Mwanzo Kwa Manabii Waliopita


Swalaah ilikuwa ni amri ya kwanza hata kwa Manabii waliopita. Alipozaliwa Nabii 'Iysaa (‘Alayhis Salaam) maneno ya mwanzo aliyotamka akiwa bado mtoto mchanga ni kuwa ameamrishwa Swalaah: Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ ۖ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا ﴿٢٧﴾
Akawafikia watu wake akiwa amembeba (mtoto); wakasema: “Ee Maryam! Kwa yakini umeleta jambo lisilopata kusikika, kuu na ovu mno. 


يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا ﴿٢٨﴾
 “Ee dada wa Haaruwn! Hakuwa baba yako mtu muovu, na wala hakuwa mama yako kahaba.”

فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ ۖ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا ﴿٢٩﴾
Akamuashiria. Wakasema: “Vipi tuseme na aliye kwenye susu, bado mtoto?”

قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّـهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا ﴿٣٠﴾
 (Mtoto) Akasema: “Hakika mimi ni mja wa Allaah; Amenipa Kitabu (Injiyl) na Amenijaalia kuwa Nabiy.”

وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا ﴿٣١﴾
 “Na Amenijaalia kuwa mwenye kubarikiwa popote nitakapokuweko, na Ameniusia Swalaah na Zakaah madamu niko hai.”  [Maryam: 27-31]

Nabii Muwsaa (‘Alayhis Salaam) pia alipoanza tu kupewa risala, ilikuwa ni ukumbusho wa Swalaah: Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَهَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ ﴿٩﴾
Na je, imekufikia hadithi ya Muwsaa?


إِذْ رَأَىٰ نَارًا فَقَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِقَبَسٍ أَوْ أَجِدُ عَلَى النَّارِ هُدًى ﴿١٠﴾
Alipouona moto akawaambia ahli zake: “Bakieni (hapa); kwa yakini nimeona moto, huenda nikakuleteeni kutoka humo kijinga cha moto, au nipate kwenye huo moto mwongozo.

فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ يَا مُوسَىٰ ﴿١١﴾
Basi alipoufikia, aliitwa: “Ee Muwsaa!

إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى ﴿١٢﴾
 “Hakika Mimi ni Rabb wako; basi vua viatu vyako, kwani wewe hakika uko katika bonde takatifu la Twuwaa.

وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَىٰ ﴿١٣﴾
 “Nami nimekuchagua; basi sikiliza kwa makini yanayofunuliwa Wahy (kwako).

إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي ﴿١٤﴾
 “Hakika mimi ni Allaah hapana Muabudiwa wa haki ila Mimi; basi niabudu, na simamisha Swalaah kwa ajili ya kunidhukuru. [Twaahaa: 9-14]


Nabii Ismaa'iyl (‘Alayhis Salaam) amesifiwa kwa kuamrisha watu wake Swalaah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِسْمَاعِيلَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صَادِقَ الْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا ﴿٥٤﴾
Na mtaje katika Kitabu Ismaa’iyl. Hakika yeye alikuwa mkweli wa ahadi na alikuwa Rasuli na Nabiy.

وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِ مَرْضِيًّا ﴿٥٥﴾
Na alikuwa akiwaamrisha ahli zake Swalaah na Zakaah, na alikuwa mridhiwa mbele ya Rabb wake. [Maryam: 54-55]


Hivyo basi Swalaah ni ‘ibaadah iliyo muhimu kupita zote kutokana dalili hizo na pia kwa ajili ya uhusiano wetu na Rabb wetu Aliyetuumba  Akatuamrisha kumwabudu Yeye pekee kama Anavyosema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾
Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. [Adh-Dhaariyaat: 56]


0 Comments