Askari wa Israel wavamia Msikiti wa al Aqsa, wawazuia Waislamu kuswali Ijumaa

Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamevamia Msikiti mtukufu wa al Aqsa na kuwajeruhji Wapalestina wengi katika viwanja vya msikiti huo wakiwazuia kutekeleza ibada ya Swala ya Ijumaa.
Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa, wanajeshi wa Israel wamevamia msikiti huo katika jaribio la kuwazuia Wapaletina kutekeleza Swala ya Ijumaa. Askari hao waliwafyatulia risasi Wapalestina hao na kujeruhi baadhi yao. Waumini wengine kadhaa wemetiwa nguvuni.
Mapema leo pia Wazayuni wa Israel wamevamia msikiti mwingine katika eneo la Beit Safafa karibu na Quds inayokaliwa kwa mabavu na kuuchoma moto. Vyombo vya habari vya Israel vimedai kuwa, moto huo hausababisha hasara za nafsi.
Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamekuwa wakivamia na kuushambulia mara kwa mara Msikiti wa al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Mashambulizi ya leo na wanajeshi wa Israel dhidi ya Msikiti wa al Aqsa yamefanyika wakati Rais Donald Trump wa Marekani akijitayarisha kuzindua mpango wake uliopewa jina la "Muamala wa Karne". Mpango huo umekataliwa katakata na Wapalestina.

Msemaji wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Nabil Abu Rudaineh, amesema kuwa, mpango huo wa Trump una nia ya kutokomeza na kuzika kabisa kadhia ya Palestina.  

0 Comments