Medical Insurance Halaal Au Haraam?

SWALI LA KWANZA:
  
Bismilahi warahmatulahi wabarakatu Asalamu Aleykum Warahmatulahi Wabaraakatu, Shukran kwa kazi kubwa munayofanya.

Ama swali yangu ni kuhusu medical insurance? Nilikuwa nataka kuweka mtoto wangu katika medical insurance ili akigonjeka walipe bill yake. Huwa wanaitisha alfu 25 kwa mwaka alafu wanalipa bill ya mtoto akikonjeka hata kama bill ni kubwa. Medical insurance ni halali ama haramu??? Shukran


SWALI LA PILI:

Bismillahi Rahmani Rahiim.
Shukran sana kwa kazi nzuri munayo fanya. Swali yangu je medical insurance ni halali ama haramu?? Kwa mfano nalipa 25,000 khs kwa mwaka. Na kampuni hii itagarimia bill ya hospital kwa muda wa mwaka moja. Hata kama itakuwa ni pesa nyingi watalipa na pia naweza kuchagua ni hospitali gani ninapenda kutibiwa bila kujali pesa. Je medical cover hii ni halali???


 JIBU:

 Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.


Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu uhalali au uharamu wa medical insurance.
Misingi ya insurance imejengwa katika uharamu hivyo kuifanya kuwa haramu katika sheria yetu ya Kiislamu. Insurance ni bahati nasibu na kwa ajili ya kutaka kupata faida nyingi huwa hawakubali mtu ambaye ana ugonjwa wa kudumu kujiandikisha.

Insurance ni bahati nasibu, kwa kuwa unaweza usiwe mgonjwa kwa mwaka mzima hivyo kufanya pesa zako ziwe zimepotea bila huduma ya aina yote. Uislamu haufanyi kazi aina hiyo, unataka mtu atoe pesa na apate huduma kutoka kwa shirika au kampuni au idara nyingine yoyote. Kisha pia katika insurance huwa kuna riba ndani yake na udanganyifu ambao umekatazwa na Uislamu.

Ikiwa kampuni ndio inalipa gharama ya wewe kwenda kutibiwa na hakuna njia nyingine utachukua insurance hiyo. Hata hivyo, ikiwa kampuni au shirika ni la Muislamu inafaa uzungumze na wakubwa kuhusu njia mbadala ya hiyo ya haramu. Na njia moja ni mwajiri kulipa tu wakati mfanyakazi ni mgonjwa na anapokwenda hospitali kutibiwa. Njia hii itakuwa ni afadhali sana kujiepusha na haramu. Na lau kampuni itakuwa ni asiyekuwa Muislamu yeye hawajibiki na sheria ya Kiislamu, na lau hiyo itakuwa ni huduma kampuni inayotoa utaichukua kwani itakuwa si wewe uliyeingia katika hilo wewe kwako ni kupata huduma ya matibabu unapokuwa mgonjwa.

Na Allaah Anajua zaidi

0 Comments