Al-Lajnah Ad-Daa'imah: Maana Ya At-Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah Na Al-Uluwhiyyah

Maana Ya At-Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah Na Al-Uluwhiyyah

Al-Lajanah Ad-Daaimah


SWALI:

Nini maana ya Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah na Al-Uluwhiyyah?

JIBU:

Maana ya Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Tawhiyd ya Uola):  Ni mja kumpwekesha Allaah Aliyetukuka na Mtukufu kwa vitendo Vyake kama kuumba, kuanzisha uumbaji,  kuruzuku, kuhuisha na kufisha.
Maana ya Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (Tawhiyd ya ‘Ibaadah): Ni mja kumpwekesha Allaah kwa vitendo vyote ‘Ibaadah kama; du’aa, kuomba msaada, kuomba uokozi, kukhofu, kutaraji matumaini, kutawakali, na kila aina za ‘ibaadah.


Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. [Juz: 1   Uk. 6-7]

0 Comments