Fahamu jinsi ya kujikinga na Coronavirus

*Taarifa hii imetafsiriwa toka Tovuti ya Idara ya Kudhibiti Magonjwa Marekani (CDC) kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili duniani.*

Mpaka sasa hakuna tiba wala chanjo ya Coronavirus. Njia nzuri zaidi ya kupambana na ugonjwa huu ni kuepuka mwingiliano na watu wenye ugonjwa huo. Hata hivyo CDC inashauri kuhusu hatua za kuchukua kila siku kuzuia msambao wa virusi hivyo vinavyoathiri mfumo wa upumuaji. Hatua hizo ni pamoja na:


  • Epuka mwingiliano na watu wenye virusi vya Corona.
  • Epuka kugusa macho, pua na mdomo kwa mikono isiyooshwa vizuri. 
  • Usitoke nyumbani kama unahisi kuumwa.
  • Funika mdomo wako kwa kutumia tishu wakati unapopiga chafya na tupa tishu hiyo katika eneo maalumu.
  • Safisha kwa dawa za kuua vimelea vya magonjwa maeneo yote ambayo yanaguswa mara kwa mara nyumbani na maeneo ya kazi mfano vitasa vya milango, viti, chuma za kwenye ngazi (handrails) na kadhalika.
  • Tumia “mask” kufunika pua na mdomo inapobidi na hasa kwa watu ambao wanahudumia wagonjwa au watu wenye dalili ya kuugua. 
  • Nawa mikono yako kwa maji na sabuni walau kwa sekunde 20 hasa baada ya kwenda chooni, kabla ya kula, baada ya kupenga kamasi, kukohoa au kupiga chafya. Kama maji hayapatikani kirahisi tumia sanitizer. Daima nawa mikono yako kwa maji na sabuni. 

0 Comments