India yasema Marekani na wengine watilia siasa ghasia za kidini

India leo imewashtumu wakosoaji wake miongoni mwao jopo la serikali ya Marekani na shirika la ushirikiano wa Kiislamu kwa kutokuwajibika na kuingiza siasa katika ghasia za mjini New Delhi ambazo zimesababisha vifo vya watu 35. Katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Delhi ambayo yameshuhudia ghasia kali na visa vyo kuzichoma moto mali, hali ya utulivu ilirejea kiasi huku maafisa wa polisi na wa kijeshi wakishika doria, na maafisa wakuu serikalini wakitoa wito wa amani. 

Makabiliano kati ya waungaji mkono na wapinzani wa sheria mpya ya uraia inayokabiliwa na utata, yaligeuka kuwa ghasia kali kati ya jamii ya kihindu na waislamu. Sheria hiyo inarahisisha zoezi la kupata uraia wa India kwa makundi ya dini za wachache katika nchi zenye Waislamu wengi, bila kuwahusisha waislamu kutoka nchi hizo. Kumekuwa maandamano nchini India tangu kupitishwa kwa sheria hiyo na bunge mwezi Desemba. Polisi inasema takriban watu 130 wamekamatwa kufikia sasa kuhusiana na ghasia hizo za mjini New Delhi.

0 Comments