Saudi Arabia yapiga marufuku Kupiga Self katika misikiti mitukufu, Masjid Al Haram na Masjid An Nabawi


Mamlaka ya Serikali ya Saudia imeweka kizuizi juu ya kuchukua/kupiga picha za selfies katika Sehemu hizi mbili Takatifu. Ripoti mbali mbali zimetoka kuthibitisha ukweli wa habari hii.
Gazeti la Daily Sabah la Uturuki liliripoti kwamba Mamlaka ya Saudia imepiga marufuku tangu Novemba 12, 2017, na pia Jarida la Jakarta la Indonesia lilichapicha habari hii mnamo tarehe 27 Novemba, 2017 kuwa Mamlaka ya Saudia, Mamlaka ya Saudia imepiga marufuku upigaji wa picha za selfi kwenye Misikiti hiyo miwili.

Myahudi huyo mzaliwa wa Urusi, Ben Tzion alionekana amesimama ndani ya MASJID AN NABAWI, Madina uku akichukua selfies na maeneo mengine ya Kihistoria ndani ya Masjid Al Haram na maeneo mengine ambayo Wasio Waislamu hawaruhusiwi kufika.

Mamlaka ya Saudia ilichukua hatua hiyo baada ya kuonekana kwenye mitandao picha za selfie zilipigwa na Myahudi akiwa Makka na Madina! Picha ambazo zilizua mabishano mengi na maswali dhidi ya Serikali ya Saudia kwa vipi Mtu asiye Muislamu kupata nafasi ya kuingia mahali ambapo Wasio Waislamu hawaruhusiwi.
Kabla ya hapo, kulipatikana video ya Wachumba wawili kutoka Uturuki, wakiwa mbele ya AlKaaba, huku ikimuonyesha mwanamme akimpigia magoti mwanamke ishara ya kutaka udhibitisho wa uchumba wao na kuvishana pete (Marriage proposal), tendo ambalo lilileta shida kubwa kwa serikali ya Saudia na waumini wa Kiislamu walio tazama video ile.

Kwa kuongezea, Mamlaka ya Saudia ilisema kwamba uchukuwaji wa picha za Selfies zinasababisha usumbufu mkubwa kwa waumini wengine. Na kwa atakayepatikana akifunja amri hii, hatua za kisheria zitachukuli na atanyang’anywa kamera au simu yake au kifaa anachokitumia kupigia picha hizo za selfi.

Vile vile, mamlaka ya Saudia imesema kuwa, marufuku hiyo itasaidia waumini wa Kiislamu kuzingatia lengo na kiini halisi cha Umrah na Hajj, lengo ambalo lilikuwa lishaanza kupotea kwa baadhi ya Waumini ambao, kwenda kwao Umrah/Hijjah kumekuwa ni kama maonyesho na kutafuta sifa mitandaoni. Habari hii kwa mara ya kwanza ilitoka mitandaoni mwezi Novemba, 2017,

Kuanzia sasa, kuchukua picha za selfies ni marufuku kabisa katika Miji miwili Mitakatifu na Waislamu wote ulimwengu lazima kufuata na kutii sheria hii, ili lengo la kufanya umrah na hajj litimie.

0 Comments