Habari za hivi punde : Sheikh Nyundo Amefariki Dunia Leo Alfajir

Sheikh Hussein Hassan Jaku maarufu Sheikh Nyundo amefariki Dunia asubuhi katika hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar.

Taarifa zilizothibitishwa na jamaa wa karibu wa Sheikh Nyundo zinasema ni kweli amefariki katika hospitali ya Mnazi mmoja baada ya kulazwa kutokana na kuugua ghafla.

Maziko yanatarajiwa kuwa leo hii Kidongo Chekundu Msikiti Shurba.

Uongozi na wafanyakazi wote wa Muislamu blog tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na waislam wote kwa msiba huu mzito wa Sheikh Nyundo. Inna lillah wa inna ilayh rajiuwn, Mwenyezi Mungu amlipe kheri kubwa kwa mema yake na amsamehe madhambi yake.

Credit : Zanzibar24

0 Comments