Mufti wa Tanzania atoa maelekezo 11 kwa Waislamu

Katika kukabiliana na kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona (CODIV-19), Baraza la Ulamaa nchini Tanzania limetoa maelekezo 11 kwa Waislam wote.
Pamoja na maelekezo hayo, baraza hilo litachukua hatua zaidi endapo kasi ya maambukizi itaongezeka nchini humo na kuhatarisha maisha ya Watanzania.

Maelekezo hayo ni pamoja na kufunga madrasa zote kufutia agizo la Serikali la kusitisha masomo kwa shule na vyuo vyote hadi hapo itakapotangazwa.
Pia, baraza hilo limewataka Waislam kutii amri ya karantini pale itakapotolewa na mamlaka husika ili kuokoa nafsi zisiangamie.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir ametoa maelekezo hayo leo Jumatano Machi 18,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akisema ni muhimu kuzingatia agizo la kuacha misongamano ili kuzuia ugonjwa huo usisambae.

“Kuokoa nafsi za wengine zisiangamie ni ibada kubwa na mtekelezaji wa amri na maagizo haya atalipwa thawabu zisizo kifani. Atakayepinga amri hizi akasababisha watu kuambukizwa na kufa ataandikiwa dhambi,” amesema

0 Comments