Fataawaa: Mukhtasari Wa Fataawaa Kuhusu Yanayobatilisha Na Yasiyobatilisha Swawm

Yafuatazo Ni Mukhtasari Wa Mas-alah Ambayo Aghlabu Huulizwa Khaswa Katika Ramadhwaan Kuhusiana Na Swawm


1-At-Tahaamiyl: (Suppository) Dawa Za Kuteremsha Homa Zinazowekwa Kwa Njia Ya Utupu Wa Nyuma

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Imaam ibn ‘Uthaymiyn]2-Dawa Ya Macho Ya Maji (Eye Drops)

Hukmu Yake: Haibatilishi. Lakini atakapohisi ladha ya hiyo dawa kwenye koo lake, basi kiakiba akilipa hiyo siku ni bora.

[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn]

3-Wanja Wa Macho

Hukmu Yake: Haibatilishi na lakini ni bora atumie usiku baada ya kufuturu.

 [Ibn ‘Uthaymiyn, Ibn Baaz]4-Dawa Ya Kudondoshea Masikioni

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]5-Kipulizo Cha Pumu.

Hukmu Yake:  Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn, Al-Lajnah Ad-Daaimah]6-Kipulizo; Mashine Ya Kuvuta Hewa (Oxygen)

Hukmu Yake: Haibatilishi kwa kuhitajika kwa dharura.

[Ibn ‘Uthaymiyn]
7-Sindano Ya Penicillin

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
8-Sindano Ya Insoline Kwa Mgonjwa Wa Kisukari

Hukmu Yake:  Haibatilishi.

 [Ibn ‘Uthaymiyn, Ibn Baaz]
9-Sindano Ya Ganzi Kwa Ajili Ya Kung’olewa Jino Na Kuweka Mjazo Wa Meno Na Kusafishwa Meno

Hukmu Yake: Haibatilishi. Lakini atahadhari kumeza chochote katika dawa na damu (kwa maana akimeza atabatilisha Swawm).

[Ibn Baaz]10-Kutumia Manukato Mazuri Na Kuyanusa

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
11-Kunusa Harufu Ya Udi Uliofukizwa

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
12-Dawa Ya Kulainisha Mdomo (Lip Balm)

Hukmu Yake: Haibatilishi, kwa sharti kwamba asimeze kitu.

[Ibn ‘Uthaymiyn]
13-Vipodozi (Make Up)

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

Tanbihi: Mwanamke hapaswi kujipamba kudhihirisha mapambo yake kwa wanaume ajnabiy wasio mahaarim wake.
14- Kuvuja Damu Pua Na Kun’goa Jino Huku Damu Ikitoka

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
15-Kutolewa Damu Kwa Ajili Ya Kipimo

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
16-Kuota Kitendo Cha Ndoa Na Kutokwa Manii

Hukmu Yake: Haibatilishi

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

17-Kutokwa Na Madhii. (Madhii Ni Maji Mepesi Mno Yenye Kunatanata Yanayotoka Wakati Wa Matamanio Ya Kimwili)

Hukmu Yake: Haibatilishi

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
18-Kuogelea Na Kupiga Mbizi

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
19-Dawa Ya Kusukutua

Hukmu Yake: Haibatilishi kwa sharti kuwa asimeze kitu.

[Ibn ‘Uthaymiyn]
20-Kutumia Mswaki

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]

Lakini ni mswaki wa kawaida na si ambao una ladha.
21-Dawa Ya Kusafisha Meno

Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa haitomezwa ikaingia tumboni. Na lililo salama zaidi ni kutokuitumia kwa sababu ina nguvu kali.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
22-Kumeza Makohozi

Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa haitofikia mdomoni. Ama ikifikia mdomoni akameza, basi inabatilisha Swawm.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
23-Kuonja Chakula

Hukmu Yake: Haibatilishi lakini bila ya kumeza na wala asifanye mtu isipokuwa kwa dharura.

 [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
24-Vidonge Vinavyoweka Chini Ya Ulimi Kwa Kutibu Maradhi Ya Moyo

Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa havitoyeyuka na kumezwa mate yake ambayo yameyeyuka ndani ya mdomo. Hakika vinabatilisha Swawm. Lakini vikiwa haviyeyuki na havimezwi, basi havina madhara.

[Ibn ‘Uthaymiyn]25-Dawa Ya Kudondoshea Puani

Hukmu Yake: Inabatilisha ikifikia tumboni [akimeza].

[Ibn ‘Uthaymiyn]

Dawa ya pua haifai kwa mwenye Swawm na atakayetia ikafikia kooni akasikia ladha yake, basi alipe Swawm yake.
26-Viraka Vya Nikotini (Vya Kubandika Mikononi Au Mabegani Kusaidia Wavutaji Sigara Waache Uvutaji)

Hukmu Yake: Inabatilisha.

[Al-Lajnah Ad-Daaimah]
27-Hijaamah (Kupigwa Chuku, Kuumikwa)

Hukmu Yake: Inabatilisha.
(Lakini Wanachuoni wengine wanaonelea ikiwa haitomdhoofisha anayefanyiwa Hijaamah, basi haibatilishi).

 [Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]28-Kuchangia Damu

Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa ni nyingi (na kumdhoofisha mtoaji damu) kama vile kiasi cha damu ya Hijaamah.

 [Ibn ‘Uthaymiyn]
29-Damu Inayotoka Katika Kidonda

Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa si kwa khiari yake kama vile kutolewa damu nyingi kwenye mishipa kwa ajili ya vipimo, lakini ikiwa ni kwa dharura bila ya khiari yake basi haibatilishi.
30-Kutapika Kwa Makusudi

Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa kwa makusudi. Ikiwa si makusudi haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
31-Sindano Ya Kuingiza Chakula Kupitia Maji Mwilini Kumtia Mtu Nguvu

Hukmu Yake: Inabatilisha.

Ama sindano ya misuli au ya mishipa au ya ngozi haibatilishi. Na ni salama zaidi kufanya usiku baada ya kufuturu.

[Ibn ‘Uthaymin, Ibn Baaz]32-Kuvuta Harufu Ya Moshi Wa Udi

Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa anajua, ama ikiwa kunusa tu haibatilishi.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
33-Kujichua (Masturbation)

Hukmu Yake: Haijuzu katika Ramadhwaan wala nje ya Ramadhawaan na inabatilisha Swawm.

[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
34-Kudungwa Sindano

Hukmu Yake: Haibatilishi. Ama ikiwa ni kwa ajili ya kuingiza chakula au nguvu ya chakula (kama glucose) inabatilisha. Na usalama zaidi kutumia usiku [baada ya kufuturu].

[Ibn Baaz]35-Kupaka Hinna

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn ‘Uthaymiyn]36-Kula Au Kunywa Kwa Kusahau

Hukmu Yake: Haibatilishi, lakini mtu anapokumbuka tu aachilie mbali hata kama kimo mdomoni akiteme.

[Ibn ‘Uthayimyn].37-Kuvuta Sigara

Hukmu Yake: Inabatilisha na ni haramu wakati wowote katika Ramadhwaan na nje ya Ramadhwaan.

[‘Ibn ‘Uthaymiyn]38-Kuoga

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn ‘Uthaymiyn]39-Kumeza Chakula Kilichokuja Kwa Kucheua

Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa chakula au maji aliyocheua yatafika mdomoni akameza, ama ikiwa yameishia kooni basi hana juu yake chochote

[Ibn ‘Uthaymiyn]40-Kusafishwa Damu Ya Mafigo (Dialysis)

Hukmu Yake: Inabatilisha na inampasa alipe Swawm yake.

[Ibn Baaz]41-Maongezi Maovu Ya Haramu

Hukmu Yake:  Hayabatilishi lakini thawabu zitapunguka  na kama yanahusiana na haki ya mtu (Kumtusi mtu), basi itampotezea kabisa thawabu za Swawm.

[Ibn Baaz]42-Kumeza Mate

Hukmu Yake: Haibatilishi.

[Ibn Baaz]43-Kumeza Maji Wakati Wa Wudhuu

Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa si kwa kukusudia.

[Al-Lajnah Ad-Daaimah]

0 Comments