Mufti wa Tanzania awataka waislamu kufanya dua kwaajili ya corona

MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Ali amewataka waislamu wa taasisi na madhehebu yote,  wake kwa waume kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dkt. John Magufuli la kuwataka watanznaia kwa kila mmoja na Imani yake kumuomba Allah kwa unyenyekevu mkubwa atuondolee janga la Corona.

Mufti wa Tanzania amewaagiza masheikh wote wa mikoa,  wilaya,  kata na maimamu wa misikiti yote nchini kwenye swala ya Ijumaa waongoze dua maalum kwa unyenyekevu mkubwa kumlilia Allah huku wakizingatia Mola ni muweza na wawe na matarajio ya kukubaliwa dua.

Mufti amewataka waislamu kutumia hizi kumuomba Mwenyezi Mungu wakiwa msikitini,  Nyumbani au maeneo yao ya kazi...
Amewataka waislamu kufanya maombi hayo huku wakizingatia kanuni na maelekezo ya wataalamu maeneo ya ibada ikiwa ni pamona na usafi wa hali ya juu na kuchunga umbali pamoja na kufupisha ibada

0 Comments