Mkuu wa wilaya awataka wananchi kusherekea Eid majumbani mwaoMkuu wa wilaya ya kaskazin ‘B’ Rajab Ali Rajab amewataka wananchi katika wilaya yake kusherehekea skuu ya eid el fitri nyumbani ili kuepusha maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Amesema licha ya wilaya hiyo kuwa salama hadi sasa lakini bado ipo haja kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha watoto wao wanajiepusha na mikusanyiko ambayo inaweza kusababisha maambukizi.

Akizungumza na watendaji wa wilaya hiyo ofisini kwake mahonda Rajab alisema jumla ya watu 60 wamewekwa Karantini ya wiki tatu na wote wapo salama hivyo ni vyema kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.

Alisema serikali ya wilaya kupitia kamati ya ulinzi na usalama itakuwa makini katika kipindi chote cha sikukuu kwa kuhakikisha hakuna kiwanja cha sikukuu kitakacho sherehekewa siku ya eid el fitri.

Aidha aliwataka watendaji wa wilaya hiyo kuisaidia serikali kwa kutumia nafasi zao katika jamii kwa kuhakikisha wanaelimisha kuhusu kujikinga na maambukiz ya covid 19.

Hata hivyo bwana Rajab amewataka watendaji hao kusameheana katika kipindi hiki cha kumi la mwisho la mwezi wa ramadhani pamoja na kuongeza bidii kwa kufanya ibada ili kufikia malengo ya funga.

0 Comments