May 22, 2020

Mzee Yusuph adaiwa Milioni 200, nyumba zake kuuzwa

Mzee Yusuph ameeleza kuwa ni kweli ana deni la Tsh milioni 202, na amegundua hilo baada ya miaka miwili kuchukua mkopo wa kiislam ambao baadaye umetoka kiharamu.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mzee Yusuph amesema kwenye deni hilo hajala hata mia, ila anafuatilia kesi hiyo na atapata haki yake kwani ameshampata mwanasheria japo kesi imepangwa kupelekwa mahakama kuu.

"Ni kweli nadaiwa ila kuna vitu vingine vimeongezeka,  nilichokuwa nafikiria kwenye kudaiwa kwangu ni haikuwa halali kwa sababu kuna ujanja ujanja umetumika katika akaunti yangu kwa kutoka milioni 202 bila ya mimi kuhusika, nilikuwa nataka mwanasheria anayejua kucheza na hizi kesi na sio kama naogopa, hata wakiniuzia nyumba zangu sawa" ameeleza Mzee Yusuph

"Kama ningepata mtu ambaye naweza nikamuhadithia hili jambo halafu akanaisaidia ingekuwa safi, lakini sitaki kusaidiwa pesa maana miaka hii imekuwa migumu maana nilikuwa na raha naongea hadi na Rais" ameongeza

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only