Jeshi la Myanmar laanzisha hujuma na mashambulio mapya dhidi ya Waislamu WarohingyaHarakati za jeshi la Myanmar zilizofanywa kwa lengo la kuanzisha operesheni mpya ya uvamizi na hujuma katika jimbo la Rakhine, ambalo wakaazi wake ni Waislamu, zimesababisha maelfu ya wakazi wa eneo hilo kulazimika kuyahama makazi yao na kuwa wakimbizi.

Shirika la habari la ISNA limeripoti kuwa serikali ya Myanmar imethibitisha leo kuwa jeshi la nchi hiyo limeanzisha operesheni ya hujuma na mashambulio katika maeneo ya Waislamu wanaoishi katika jimbo la Rakhine na kudai kwamba operesheni hiyo inafanyika kwa lengo la kukandamiza makundi ya wanamgambo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Usalama na Ulinzi wa Mipaka katika jimbo la Waislamu la Rakhine Min Tan, operesheni hiyo ya mashambulio ya jeshi inaweza kuchukua muda wa wiki nzima na kwamba mtu yeyote atakayekuwa amebaki katika eneo hilo atachukuliwa kama mlengwa.
Waislamu madhulumu Warohingya wakiwa katika maisha ya ukimbizi

Tangu Agosti 2017 hadi sasa, zaidi ya Waislamu elfu sita Warohingya wameuliwa na wengine wapatao milioni moja wamekimbilia nchi jirani ya Bangladesh na kuwa wakimbizi kutokana na mashambulio ya jeshi la Myanmar na mabudha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wa nchi hiyo.

Tume huru ya kutafuta ukweli ya Umoja wa Mataifa imelaani na kulikosoa vikali jeshi la Myanmar kwa jinai lilizofanya za mauaji ya halaiki na ubakaji dhidi ya Waislamu Warohingya.

0 Comments