Misri yafungua misikiti baada ya miezi minne

Misri imetangaza kufungua misikiti na makanisa kote katika nchi hiyo kuanzia Juzi Juni 27 lakini kwa kuzingatia masharti makali ya kiafya ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa tovuti ya Al Ahram serikali ya Misri pia imeondoa sheria ya kutotoka nje usiku ili kupunguza athari mbaya za kiuchumi zitokanazo na janga la COVID-19.Kwa mujibu wa sheria mpya misikiti ambayo pamoja na makanisa ilifunguwa kuanzia Machi itafunguliwa tena kwa kuzingatia sheria mpya za kiafya.

Kati ya sheria mpya za kutumia misiki ni pamoja na kuwashurutisha waumini kuvaa barakoa, kuja misikiti wakiwa na zulia au msala binafsi na kushika wudhuu nyumbani au maeneo mengine lakini si msikitini. Aidha vyoo vya misikiti vitafungwa, ni misikiti mikubwa tu itakayofunguliwa na maeneo ya wanawake hayatafunguliwa.
Watoto pia hawataruhusiwa kuingia misikitini. Halikadhalika waumini wametakiwa wasikaribiane wakati wa swala na alama maalumu zimewekwa ili kuainisha sehemu ya kusimama wakati wa kuswali.

Misri imeshuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya COVID-19 ambapo kufikia Ijumaa watu 62 ,755 walikuwa wamebukizwa huku 2,620 wakifariki dunia.

0 Comments