Agoma kula kupunga mateso ya waighur

Muanzilishi wa taasisi ya Quilliam nchini uingereza majid nawaz amesema kuwa ameanza mgomo wa kula ili kupunga mateso wanayopitia waislamu wa Uighur nchini china, Nawaz alisema kuwa lengo lake ni kuchochea mjadala ndani ya bunge la uingereza wa vikwazo kuwekwa kwa watu binafsi ambao wanahusika na ukiukwaji wa haki za binaamu.

alisema kuwa mgomo wake huo utaendelea mpaka maombi yake kwenda katika bunge la uingereza  yatakapofikisha saini 100,000 ambazo zinatosha kushinikiza mjadala katika bunge la uingereza.

pia nawaz alitoa wito kwa taasisi za kiislam kumuunga mokono, ingawa mpaka sasa taasisi hizo hazijasema kitu. Nawaz ambae anatajwa kuwa muislamu mtata nchini humo alisema kuwa dunia imefumbia macho mateso ya waislamu wa uighur ambayo yanaendeshwa na serikali ya china.

Hata hivyo taasisi yake imeshindwa kuungwa mkono kwa kuwa baadhi ya waislamu wenzake wanamuona kuwa ni mtu wa misimamo mikali, ingawa Nawaz amejitetea kuwa taasisi yake inapinga misimamo mikali.

pia Nawaz na taasisi yake amekosa uungwaji mkono kwa kuwa hajawahi kuzungumzia mdhila ya waislamu wa nchi nyingine, na hivyo anaonekana kama anafuata mkumbo wa sera za ubepali mamboleo.

Akizungumza na mtandao wa 5Pillars, Naibu mhariri, Dilly Hussein alisema: "Ni lini maajid nawaz aliwahi kulaani kitendo cha wapalestina kufukuzwa katika majumba yao huko ghaza na kwa miaka mingi wamekuwa wakipigwa mabomu na waisrael? zilikuwa wapi hasira zake za kuwatetea waislamu wa kashmir, iraq, somali, yemen na afghanistan?

aliongeza mhariri huyo: " lakini ghafla tu , maajid anaanzasha kampeni ya kuipinga china. hali hiyo inakuja kutokana na ajenda za nchi za kibepali mamboleo kuipinga china."

0 Comments