عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم، أنه قال: ((مَنْ صَلَّى الفَجْرِ في جَماعَةٍ ثُمَّ قَعَدَ يَذْكُرُ الله تَعالى حتَّى تَطْلُعَ الشَمْسُ، ثُمَّ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ كانَتْ كأجْرِ حَجَّةٍ وَعُمْرَةٍ تامَّةٍ تامةٍ تامةٍ)) أخرج الترمذي وصححه الألباني
Imetoka kwa Anas kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:((Atakayeswali Alfajiri katika Jamaa'ah kisha akakaa anamkumbuka Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira
Jitahidi ndugu Muislamu kadiri uwezavyo kuchuma hizi thawabu kubwa ambazo zingelikukalifu
Hata hivyo, pamoja na ujira wote huu, tusisahau kuwa fadhila hizo hazivunji wala hazifuti fardh ya kwenda Hajj kwa mwenye uwezo, asije mtu akadhani kufanya hayo kutakuwa kumetengua wajibu wake wa kufanya Hajj au ‘Umrah.
Juu ya hivyo imethibiti katika Swahiyh Muslim kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba walikuwa wakibakia macho wakati huo hadi jua kuchomoza kwani ni wakati mja anapogaiwa rizki yake, na ni wakati wenye kheri nyingi, unampa siha nzuri ya mwili binaadamu, na kwa ujumla ni wakati wenye baraka nyingi za kila aina kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba:
عَنْ صَخْرٍ الْغَامِدِيِّ رَضِيَ الله عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اللَّهُمَّ بَارِكْ لِأُمَّتِي فِي بُكُورِهَا)) الترمذي, أحمد, أبي داود, ابن ماجه
Kutoka kwa Swakhar Al-Ghaamidiyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameomba: ((Ee Allaah, wabarikie Ummah wangu nyakati za asubuhi mapema)) [At-Tirmidhiy, Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Maajah na imethibitishwa kuwa ni Hadiyth Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy].
Ni wakati wenye Baraka tele kwani Maswahaba walikuwa wakibakia kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na wakitumia wakati huo kwa kuanzisha shughuli zao mbali mbali. Pia imesimuliwa kutoka Salafus-Swaalih kwamba Ibn 'Abbaas (Radhiya-Allaahu ‘anhumaa) alimkataza mtu kulala nyakati hizo kwa vile ni wakati wa kugaiwa rizki.
Ibnul-Qayyim (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake 'Zaad Al-Ma'aad' amesema: "Usingizi wa asubuhi unanyima rizki kwani huo ni wakati ambao Muumba anaombwa rizki na wakati wa kugaiwa rizki. Hivyo usingizi unanyima rizki isipokuwa kwa dharura. Usingizi wakati huo pia ni madhara kwa mwili…"
Pia, wakati huo pamoja na baina ya Swalaah ya Alasiri na kuzama jua ni nyakati ambazo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameamrisha kumsabbih:
وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ
Na mtakase kwa kumhimidi Mola wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. [Qaaf: 39].
Tujitahidi kutekeleza hayo tukimuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atupe tawfiyq na Atutakabalie.
0 Comments