July 23, 2020

Jamii ya kimataifa yalaaniwa kwa kupuuza ukandamizaji wa Waislamu

Katika mahojiano na IQNA, Masoud Shajareh ameashiria kuhusu ukandamizaji wa Waislamu huko Kashmir nchini India na Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar na Waislamu wa jamii ya Uighur nchini China.

Ameongeza kuwa, Waislamu wa Kashmir wamekuwa wakipigania uhuru na mamlaka ya ndani kwa miongo kadhaa. Amelaani hatua ya India kuwapokonya Waislamu wa Kashmir mamlaka madogo ya  ndani waliyokuwa nayo.

Shajareh ameashiria pia kubaguliwa na kukandamizwa Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar na kusema, Waislamu nchini humo wana hali mbaya sana.

Kuhusu Waislamu wa jamii ya Uighur katika eneo la Xinjiang nchini China, mwenyekiti wa IHRC amesema wamekuwa wakiandamizwa na utawala wa China kwa muda mrefu sana. Amesema Waislamu wa jamii ya Uighur ni wapenda amani lakini wamekuwa wakibaguliwa na kukandamizwa.

Shajareh amesema IHRC imezindua kampeni kadhaa za kuwafahamisha walimwengu kuhusu Waislamu wanaokandamizwa duniani ikiwa ni pamoja na kukusanya misaada.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only