Hakuna Muislamu asiyekiri kuwa Anamependa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwani hakuna mapenzi yaliyo muhimu kabisa
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
“Sema, ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni, Allaah Atakupendeni na Atakughufirieni madhambi yenu” [Aal-‘Imraan 3: 31].
Swali kwa kila Muislamu ni: “Je, unamfuata kikweli Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?” Kwa maana; kufuata aliyoyaamrisha na kuachana na aliyoyakataza? Jibu la Swali hili ni moja tu hakuna la pili yake. Nalo ni: Kumfuata kikweli kwa kutii aliyoyaleta (aliyotuamirisha) na kuyaacha aliyotukataza; yakiwemo mafundisho yake yote na nyendo za Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) kama alivyoamuru pale alipotueleza kwamba kutatokea ikhtilaaf nyingi kama zinavyodhihirika zama hizi:
أُوصِيكُمْ بِتَقْوى اللَّه، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وإِنْ تَأَمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حبشيٌ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيرى اخْتِلافاً كثِيرا, فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وَسُنَّةِ الْخُلُفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ، عضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ، وإِيَّاكُمْ ومُحْدثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضلالَةٌ رواه أبو داود ، والترمذِي وقال حديث حسن صحيح
((Nakuusieni kumcha Allaah, usikivu na twaa hata ikiwa kiongozi wenu [Au atakayekuamrisheni] ni Mtumwa Mhabashi. Mtakaoishi miongoni mwenu mtaona ikhtilaaf nyingi. Kwa hiyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa waliongoka baada yangu. Ziumeni kwa magego [zikamateni kwa nguvu wala msiziache]. Na tahadharini na mambo ya uzushi kwani kila bid'ah ni upotofu)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy kasema Hadiyth Hasan Swahiyh].
Faida nyingine inayopatikana pindi utakapothibitisha kumfuta Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
Hakika ni faida mbili kuu anazozihitaji Muislamu kila wakati katika maisha yake.
Na katika makemeo na makatazo yake ni kuacha mambo yote ya uzushi; nayo ni
والذي نفسي بيده ما تركت شيئا يقربكم من الجنة ويباعدكم عن النار إلا أمرتكم به، وما تركت شيئا يقربكم من النار، ويباعدكم عن الجنة إلا نهيتكم عنه
((Naapa Kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko katika mikono Yake, sikuacha jambo la kukukurubisheni na Pepo na la kukuwekeni mbali na moto ila nimekwisha kukuamrisheni nalo. Wala sikuacha jambo la kukukurubisheni na moto na kukuwekeni mbali na Pepo ila nimekwisha kukukatazeni nalo)) [Silsilatul Ahaadiyth Swahiyhah]
Hao Mashia ni maadui wakubwa wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwani wanamtukania Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wake zake, wanamtukania vipenzi vyake, wanamtukania ummah wake mzima. Huku si kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bali ni kumuasi na kuwapenda maadui wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hiili ni dhahiri kwa kuonekana mashirikiano yao ya wazi na Mashia na namna wanavyoungana pamoja katika kusherehekea hizi sherehe za uzushi na kuungana katika miunganiko mingine ya uzushi kama ya mwaka mpya na Husayniyyaat (Hussein Day) katika mwezi wa Muharram ambamo ndani yake kuna maombolezo ya uzushi na uongo na vilevile kutukanwa ndani yake Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) watukufu. Bila shaka huku kunaonyesha dalili za wazi kuwa wanaofuata mwendo huo si wapenzi wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na si wapenzi wa Allaah. Kwani kwa kumuasi na kumkhalifu mafunzo yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), hapana shaka wamemkhalifu na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), na kwa hali hiyo, kama Aayah juu inavyofahamisha, hawatopendwa na Allaah.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atujaalie ni wenye kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wetu mapenzi ya kweli kweli ya dhati kwa kufuata maamrisho yake na Sunnah zake zote na kuwa mbali na bid’ah na kila aina ya uzushi na njia zozote zitakazotupeleka kumkhalifu yeye.
Post a Comment