Makumi ya maelfu ya Wapalestina wasali Sala ya Idi katika msikiti wa Al Aqsa

Makumi ya maelfu ya Wapalestina wamesali Sala ya Idul-Adh'ha katika msikiti wa Al Aqsa licha ya hatua za kiuadui zilizochukuliwa dhidi yao na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Idara ya Waqfu wa Kiislamu katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) imesema, zaidi ya Waislamu Wapalestina 27,000 walishiriki kwenye Sala ya Idi iliyosaliwa Ijumaa ya leo katika msikiti wa Al Aqsa.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Al-Qudsul-Arabi Sala hiyo ya Idi ilisaliwa huku waumini wakichunga na kuzingatia hatua zote za tahadhari kuhusiana na maambukizo ya maradhi ya Covid-19.

Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel walivamia ghafla msikiti wa Al Aqsa na kukusanya maberamu yaliyobandikwa na harakati za muqawama wa Kiislamu za Palestina kwa mnasaba wa Sikukuu hiyo ya Mfunguo Tatu.

Mufti wa Quds na Palestina Sheikh Muhammad Hussein, amesema katika hotuba za Sala ya leo ya Idi kwamba, msikiti uliobarikiwa wa Al Aqsa ni kwa ajili ya Waislamu na hakuna mvamizi au dhalimu yeyote ambaye ni mshirika wa Waislamu katika jambo hilo.

Wakati huo huo kiongozi mwandamizi wa harakati ya Hamas Khalil al Hayyah amesisitiza kuwa, Wapalestina wako tayari kujitoa mhanga roho zao kwa ajili ya msikiti wa Al Aqsa na Quds tukufu. Al Hayyah ametoa sisitizo hilo katika hotuba za Sala ya Idul-Adh'ha iliyosaliwa katika msikiti mmoja wa Ukanda wa Gaza.

Jana Alkhamisi, makundi ya Wazayuni wenye misimamo ya kufurutu mpaka yalivamia msikiti wa Al Aqsa wakati Waislamu walipokuwa kwenye visomo vya dhikri na dua katika Siku ya Arafa.../

0 Comments