Mnyanyua vyuma bingwa wa kike kutoka Latvia asilimu

Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram Bi. Koha ametangaza kuukumbatia Uislamu maishani na kisha akafuta picha zake zote za amani katika mitandao ya kijamii. Hivi sasa ukurasa wa Koha katika Instagram umesalia na picha nne tu zinazomuonyesha akiwa amevalia Hijabu.

Mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 22 ameandika: “…nawatangazia nyote kuhusu uamuzi mkubwa katika maisha yangu. Nina furaha na natoa shukrani za dhatu kutokana na uamuzi huu ambao ni sahihi. Kile ambacho naomba ni kuwa muheshimu uamuzi wangu. Hii ni siku maalumu katika maisha yangu kwa sababu kuanzia sasa mimi ni Muislamu.”

Bi. Khoha alitamka shahada mbili ambazo wanaosilimu wanatakiwa kutamka aliongeza kuwa:  “Naamini huu ni ukurasa mpya katika maisha yangu.”

Halikadhalika Bi. Koha amewaomba watu wasisambaza picha zake za zamani katika mitandao ya kijamii.

0 Comments