Moto umeteketeza Shule ya Kinondoni Muslim

Madarasa 11 kati ya 15 ya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim iliyoko Kinondoni Shamba Jijini DSM yameteketea kwa moto.

Mbali ya majengo hayo vifaa na samani za shule hiyo vimeteketea kwa moto huku Walimu na Wanafunzi wote wa shule hiyo wapatao 218 wakisalimika.

Maafisa wa Jeshi la Zimamoto wamesema ni muhimu maeneo yote ya shule yakawa na maji ya dharura ili kujikinga na madhara ya moto.

Msaidizi wa Mkuu wa Shule amesema “hali ya Watoto ipo vizuri hakuna alieathirika ila vitu vyote vimeteketea, hakuna kilichobaki na madarasa yote 11 kati ya 15, masomo yataendelea tuna Shule nyingine watahamishiwa Shule nyingine ya kwetu”.

0 Comments