July 29, 2020

Mtafiti wa Ethiopia akusanya vitabu vya kale vya Kiislamu

Hassan Mohammad Kav amesema Ethiopia ina turathi tajiri ya nakala za kale za Kiislamu na Kiarabu za karne kadhaa zilizopita ambazo zinaashiria uhusiano wa kina wa nchi hiyo ya Afrika na ulimwengu wa Kiarabu.
Ethiopia ilikuwa mwenyeji wa maswahaba wa Mtume Muhammad SAW wakati wa Hijrah ya Mtume huyo wa Uislamu kutoka Makka kwelekea Madina na hivyo ina turathi nyingi za Kiislamu ambazo zinahifadhiwa katika Jumba la Mkumbusho la Bilal mjini Addis Ababa.
Kati ya nakala za Qur’ani ambazo zimekusanywa na mtafiti huyo ni aya za Qur’ani Tukufu , tafsiri ya Qur;ani, Hadithi, na fatwa zilizoandikwa na wanazuoni wa Kiislamu Ethiopia katika ngozi ya wanyama kwa Kiarabu na lugha zingine 11 za Ethiopia.
Aidha mtafiti huyo pia amekusanya nakala za vitabu kuhusu tiba ya Kiislamu, sayansi za Kiislamu, astronimia na fasihi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only