Uamuzi wa Morocco kufungua misikiti wiki ijayo

Kwa mujibu wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Morocco, uamuzi huo umechukuliwa baada ya wachunguzi kutathmini hali ya mambo. Aidha taarifa hiyo imesema misikiti yote itawajibika kuzingatia kanuni za afya zilizowekwa kuzuia kuenea corona.

Hata hivyo, swala za Ijumaa bado ni marufuku kwa sasa huku waumini ambao wanashukiwa kuwa na corona wakihimizwa wasifike misikitini.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Morocco imesisitiza kuwa waumini wanatakiwa wazingatie kanuni za afya msikitini ikiwa ni pamoja na kutokaribiana na kuvaa barakoa. Aidha waumini wametakiwa wasijikusanya makundi makundi kabla na baada ya swala huku pia wakitakiwa wasipeana mkono.

Hadi sasa watu 14,771 wameambukizwa corona nchini Morocco huku wengine 242 wakifarikia dunia na waliopona ni 11,316.

0 Comments