Ubaguzi Marekani: Mteja wa Mwislamu apachikwa jina la Daesh katika kikombe cha kahawa

Mteja mmoja wa kike Mwislamu nchini Marekani amepewa jina la kundi la kigaidi la ISIS au Daesh kwenye kikombe alichotoa oda ya kinywaji cha kahawa.

Mkasa huo wa kibaguzi ulimkuta binti huyo wa Kiislamu aliyejulikana kwa jina la Aisha katika mgahawa wa Starbucks  mjini Minnesota huko nchini Marekani.

Aisha anasema alipowasili katika mgahawa huo alitoa oda ya kahawa na kama kawaida alimtajia jina mhudumu aliyekuja kuchukua oda, lakini anasema cha kushangaza alipoletewa oda yake aliona kikombe chake kikiwa kimeandika ISISI yaani kundi la kigaidi la Daesh.

Mhudumu aliyehudumia oda ya kahawa hiyo badala ya kuandika jila lake alichukua uamuzi wa kuandika jina la kundi la kigaidi la ISIS kwenye kikombe chake, hatua ambayo ilikuwa ni kibaguzi dhidi ya mwanamke huyo Mwislamu.
Maandamano ya wabaguzi ya kupinga ujenzi wa misikiti
Kama ilivyo ada katika migahawa ya vinywaji, vikombe huandikwa jina la mteja ili kuhudumia kwa urahisi pindi oda yake inapokuwa tayari. Binti huyo mwenye umri wa miaka 19 alishangaaa mno kupokea oda yake ya kawaha huku kikombe chake kikiwa kimeandika ISIS yaani kundi la kigaidi la Daesh

Katibu wa Baraza la Kiislamu Marekani katika mji wa Minnesota Jaylani Hussein amesema kuwa,  baraza  hilo litafikisha malalamiko yake  dhidi ya mgahawa huo kwa kitendo hicho ambacho ni cha kibaguzi.

Aidha taarifa zaidi zinasema kuwa, binti huyo wa Kiislamu tayari amejaza fomu za mashtaka dhidi ya mhudumu wa mgawaha huo akieleza kwamba, kitendo alichofanyiwa kilikiuka haki za binadamu. Baadhi yya ripoti zinaeleza kwamba, mhudumu aliyehudumia Aisha anadai kwamba, hakusikia vizuri jina la mteja huyo.

0 Comments