Tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu wengi jambo ambalo wanaghafilika nalo, kuwa, wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa (anayewakilisha mtu kumchinjia), kuanzia unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah wanatakiwa wajizuie kukata nywele za mwili na kucha mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:
عن أم سلمة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ، فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ )) وفي رواية: ((فَلا يَمَسَّ مِنْ شَعَرِهِ وَبَشَرِهِ شَيْئًا))
Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)) na katika riwaaya nyengine ya Muslim (1977); ((basi asitoe kitu katika nywele zake wala ngozi yake)) [Muslim]
0 Comments