VIDEO : Shura ya maimamu yakana kutoa waraka wa uchaguzi

Amiri mkuu wa Shura ya maimamu Sheikhe Kundecha amekana Taasisi anayoiongoza kutoa waraka wowote unaohusu uchaguzi.

Kundecha amesema yeye kama kiongozi mkuu wa waislamu hana taarifa yoyote juu ya waraka unaosambazwa mitandaoni na kwamba waraka huo ni feki.

Shehe Kundecha amempongeza Rais Magufuli kwa namna anavyoongoza nchi kwa busara na hekima na hasa kwa namna alivyotuongoza katika kipindi kigumu cha Corona.

Kadhalika amemshukuru kwa kuwaruhusu wanafunzi kuendelea na masomo.

Source: Channel ten

0 Comments