Watakaokiuka sheria ya Hija Saudia kutozwa faini na kufungwa jela

Hizo ni kati ya hatua kali ambazo zimechukuliwa katika msimu wa Hija mwaka huu.

Kwa kawaida karibu Waislamu milioni mbili kutoka maeneo yote duniani hushiriki katika Ibada ya Hija lakini kutokana na sheria kali ambazo zimewekwa kuzuia kuenea ugonjwa wa corona ni watu wachache sana watakaoruhusiwa kutekeleza Ibada ya Hija mwaka huu.

Hakuna yeyote atakayeruhusiwa kushiriki katika Ibada ya Hija bila kibali maalumu. Raia wa kigeni ambao watapatikana na hatia ya kukiuka sheria za Hija watatimuliwa Saudia mara moja na kuzuia kuingia nchini humo kwa muda fulani.

Kwa kila anayekiuka sheria kwa kuwasafirisha watu wasio na kibali za Hija atatozwa fainia ya Riyali za Kisaudi 10,000 au Dola 2,666 na kifungo cha siku 15 gerezani.

Saudia imesema asilimia 70 ya watakaotekeleza Ibada ya Hija mwaka huu ni wafanyakazi wa kigeni waishio Saudia kutoka nchi 160 na waliosalia ni raia wa Saudia.

Taarifa za awali zilisema idadi jumla ya Mahujaji mwaka huu haitazidi watu 1,000 na hatua hiyo imechukuliwa ili kzuia maambukizi ya corona.

Hadi kufikia leo watu 251,000 wameabukizwa corona kote Saudia na waliofariki ni 2,486.

0 Comments